dk mahenge akihutubia

Serikali imewahakikishia wananchi wa vijiji vya Mhangazi na Kitanda wilaya ya Namtumbo kuwatatulia haraka mgogoro uliopo wa mpaka baina ya vijiji vyao na hifadhi ya taifa ya msitu wa Kipiki uliodumu kwa muda mrefu
Kauli hii ya serikali imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt.Binilith Mahenge wakati akiongea na wananchi wa vijiji vya Mhangazi na Kitanda leo alipofanya ziara ya kikazi.
Mkuu wa Mkoa amewahahikishia wananchi kuwa serikali imejipanga  kuondoa kero zinazowasumbua wananchi kuhusu mipaka ya vijiji na hifadhi za misitu zinatatuliwa mapema kwani zimedumu muda mrefu
Amesema kuwa serikali inapenda kuona wananchi wake wanaendelea na shughuli za kuwaingizia kipato kwa amani na utulivu
Akieleza chanzo cha mgogoro huu diwani wa kata ya Kitanda  Titus Ngoma amemweleza mkuu wa mkoa kuwa wanakijiji walitoa maeneo yao kwa wizara ya maliasili na utalii mwaka 2000 ili wapanue eneo la hifadhi ya Taifa ya msitu .
Amesema kutokana na wizara ya maliasili na utalii kuchelewa kuweka mipaka huku mahitaji ya ardhi kwa  wakulima yakiongezeka kulipelekea kuzaliwa mgogoro huu mwaka 2010 ambapo wizara iliaza operesheni ya kuwaondoa wakulima
 
wananchi wakimsikiliza dk mahenge
Wizara iliwaondoa tena wakulima mwaka 2014 wakiwa tayari wamelima mazoa yao ya mahindi na mbaazi kitu ambacho kimeleta matatizo yaliyokuza mgogoro huu
Akijibu malalamiko ya wananchi Dkt.Mahenge amekiri kuwa mgogoro upo na unahitaji wataalam wa misitu,ardhi na maliasili waende mapema kuongea na mwananchi na hatimaye kushauri serikali namna bora ya kuumaliza.
“Ninawasihi mtulie ili utatuzi wa mgogoro huu upatikane.Ninyi muwe tayari kutoa ushirikiano kwa serikali wakati wote wa utatuzi wa kero hii” alisema Dkt.Mahenge
Aliongeza kusema serikali inahitaji hifadhi ya msitu iendelee kuwepo lakini pia wananchi wapate eneo bora na la kutosha la shughuli za uzalishaji mali ili wajikwamue na umasikini
“Wananchi endeleeni kufanya kazi zenu za maendeleo mkizingazia sheria na taratibu za nchi ili kuimarisha uchumi wa kaya wakati serikali ikiendelea kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro huu “ alisema mkuu wa mkoa
Mkuu wa mkoa amemwagiza Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Luckiness Amlima kwenda kwenye eneo la mgogoro kufanya tathmini ya mazao yaliyo ndani ya eneo hilo la msitu na kisha asimamie wakulima wavune mazao kwa amani  bila kusumbuliwa wakati hatua za utatuzi zikiendelea kuchukuliwa.
Katika ziara hii mkuu wa mkoa aliambatana na mbunge wa jimbo la Namtumbo amabaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano,Uchukuzi na Ujenzi.
Mwisho
Revocatus Kassimba
Afisa Habari
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Ruvuma
0754448929

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO