AMEZALIWA Februari 25 hivi majuzi tu yaani mwaka 1981 lakini ameshafanyakazi ambazo zimetikisa dunia kiasi cha kutajwa katika tuzo kadha na hata kunyakua nyingine.
Kijana huyu wa juzi ambaye  pia anajulikana kama Shahid Khattar ametokea sana katika filamju zilizofanya vyema za Kihindi.
Mvulana huyu wa juzi ambaye ni mtoto wa muigizaji Pankaj Kapur na Neelima Azeem, alizaliwa mjini New Delhi hata hivyowazazio wake walitengana wakati yeye akiwa na umri wa miaka mitatu na kuendelea kuishi na mama yake.
Wawili hao waliondoka na kwenda kuishi Mumbai na akiwa na miaka 10 alijiunga na  chuo cha dansi cha Shiamak Davar. Kapoor alionwa katika filamu kadhaa kama dansa  katika filamu kadhaa za miaka ya 1990 na baadae akwia katika muziki za video na matangazo ya televisheni.
Tokeo la kwanza la  filamu  alilifanya 2003 akiwa muigizaji kinara katika simulizi la mapenzi la Ishq Vishk.
Lilikuwa bonge moja la filamu lililotikisa na kumpatia tuzo ya Filmfare muigizaji bora wa kiume.
Baada ya filamu hiyo alipata nafasi katika filamu kadhaa  zilizoshindwa kufanya vyema mpaka pale alipopata nafasi za kuicheza akiwa na Amrita Rao , Sooraj Barjatya moja ya waigizaji wanalipwa vitita vinono katika filamu moja  inayozungumza familia katika mfumo wa drama ya Vivah (2006).
Baadae Kapoor alipata heshima tena ya kutajwa katika tuzo za Filmfare kwa kufanikiwa kucheza vyema nafasi ya mfanyabiashara aliyekuwa na matatizo na msongo  Imtiaz Al katika komedia ya mapenzi ya Jab We Met (2007) na kwa filamu ya  mapacha  Vishal Bhardwaj ya Kaminey (2009).
Baada ya sinema hizo aliigiza sinema nyingine ambazo hazikufanya vyema tena kabla ya kuingia katika filamu ya aksheni ya R... Rajkumar (2013). Mwaka  2014, Kapoor aliigiza katika Hamlet nafasi ya Bhardwaj kwenye drama iliyosiofika sana ya Haider,  ambako alipata tuzo ya muigizaji bora ya Filmfare,  na mwaka huu ameigiza katika sinema ya matumizi mabovu ya dawa za kulevya akiwa mwimbaji ndani ya filamu ya aksheni inayosisimua ya uhalifu ya Udta Punjab.
Akielezwa kama mmoja ya watu mashuhuri wenye mvuto mkubwa, Kapoor amekuwa akiendelea na  umashuhuri wake pamoja na  kazi zake nyingi wakati Fulani kutofanya vyema.
Ingawa kwanza alionekana kwamba anacheza zaidi sinema za mapenzi, Kapoor kwa muda sasa amekuwa akiigiza simulizi za kusisimua na za aksheni zilizomwezesha kupata tuzo kadha zikiwemo zaFilmfare.
Kapoor amepitia shule ya Gyan Bharati huko Delhi na Rajhans Vidyalaya huko Mumbai na baadaye alienda chuo cha Mumbai cha Mithibai  kwa miaka mitatu.
Aliyemwezesha  kuingia katika sinema ni projuza mmoja ameona video ya Aryans ya "Aankhon Mein". Projuza huyo Ramesh Taurani alimuona anafaa katika sinema lakini alipokutana naye alimuona ni mdogo hafai kwenye uigizaji lakini baadae ndio akampatia nafasi katika sinema ya Ishq Vishk (2003).hapa alilazimika kufanya mazoezi zaidi ili kuujenga mwili wake.
Ishq Vishk  inauzngumzia stori ya Rajiv Mathur (Kapoor), mwanafunzi ambaye anajiingiza katika mapenzi na wanafunzi wenzake wawili wenye tabia tofauti nafasi zilizochezwa na Amrita Rao na  Shenaz Treasurywala.
Kapoor  baadae aliungana na Ghosh  katika filamu tofauti  na ile ya Ishq Vishk.Filamu hii ya Fida (2004) ilimueleza kama mwanafunzi aliyekumbwa na mahaba na mwanamke ambaye naye anamchezesha shere na mchumba wake wanamuingiza katika mpango wa kuibia benki.
Mwaka huo huo Kapoor alicheza filamu ya mapenzi ya Dil Maange More .
Mwaka  2006, Kapoor alicheza na Kareena Kapoor  kwenye filamu mbili zar 36 China Town na komedi ya Chup Chup Ke. 36 China Town, inazungumzia mauaji na  staa wetu wa leo alikuw amiongoni mwa watu saba wanaotuhumiwa.
Katika filamu ya Priyadarshan ya Chup Chup Ke, alicheza kama mwanamume mwenye usongo wa mawazo anayejifanya kuwa bubu na kiziwi.
Mwaka 2012, Kapoor  alitwaa nafasi ya Kunal Kohli's Teri Meri Kahaani (2012), akiwa na Priyanka Chopra. Humu alikuwa wanazungumzwa wapenzi ambaow aliokosanishwa kuoana katika nyati tatu tofauti.
Akiwa amecheza  filamu ya Prabhu Deva ya R... Rajkumar;  iliyoingiza fedha za India milioni 995 sawea na dola za Marekani  milioni 15 kapoor akajijengea heshima kama moja ya sinema zake kuwba zilizoingiza fedha nyingi nchini mwake na duniani.
Juni mwaka huu 2016, Kapoor amekamilisha uchukuaji opuicha wa fiklamu ya Rangoon, kama askari wa World War II, akiwa na  Saif Ali Khan na Kangana Ranaut ikiwa ni sinema yake ya tatu aliyoshirikiana na Vishal Bhardwaj.
Nje ya kazi maisha ya Kapoor yamekuwa yakiandikwa sana katika magazeti ya India.Waklati wa uchukuaji wa opicha ya Fida mwaka 2004, alianza kutoka na Kareena Kapoor na wawili haow alizungumzia uhusiano waziwazi. Walikuwa kiini cha kashifa iliyochapishwa sana ya Mid Day ambapo picha zao kadha wakibusiana zilichapishwa.
Wapenzi wawili hao waliachana mwaka 2007 wakati wa utengenezaji wa Jab We Met.
Hata hivyo anatuhumiwa kuwa na uhusiano pia na akina Vidya Balan na Priyanka Chopra.
Machi  2015, Kapoor alizungumzia ndoa yake na Mira Rajput, mwanafunzi  kutoka New delhi ambaye  amepichana naye kwa miaka 13. The Times of India  iliandika kwamba Kapoor alikutana na Rajput kupitia kundi la kidini la Radha Soami Satsang Beas. Waliona Julai7 2015 katika sherehe binafsi iliyofanyika Gurgaon.
Wawili hao wanategemea mtoto baadae mwaka huu.
Filamu zilizompa jina kubwa:
•    Ishq Vishk (2003)
•    Vivah (2006)
•    Jab We Met (2007)
•    Kaminey (2009)
•    R... Rajkumar (2013)
•    Haider (2014)
Source:Oliva Kibua,Spotileo

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO