WATU  zaidi ya 80 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya  mtu mmoja akiendesha lori alipofanya shambulio la kuwakanyaga watu waliokuwa waisherehekea siku ya mapinduzi ya Ufaransa katika jiji la Nice.
Aidha mtu huyo baada ya kuendesha gari hilo alitoka na kuanza kufanya shambulio la bunduki kabla ya polisi hawajamuua.


Haijajulijana kama kuna kundi linahusika na mauaji hayo.
Pia imeelezwa kuwa gari hilo lilikuwa na mabomu ya kutupa kwa mkono na bunduki kadhaa.
Shambulio hilo lilifanyika baada ya kufyatuliwa kwa fataki.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema shambulio hilo ni la kigaidi na pia kuongeza muda wa hali ya hatari kwa miezi mitatu zaidi.
Ufaransa imekuwa katika hali ya hatari toka lilipofanyika shambulio la kigaidi Novemba mwaka jana ambapo watu 130 waliuawa.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO