Shambulio la kujitoa mhanga kwa kutumia gari limefanyika katika Mji mtakatifu wa Medina nchini Saudi Arabia karibu kabisa na Msikiti wa Mtume.
Shambulio hilo limeoneshwa katika televisheni ya al-Arabiya TV  na gazeti la  Okaz.
Televisheni hiyo ilionesha gari linalowaka moto: Hata hivyo  hakuna taarifa rasmi kuhusu tukio hilo kutoka kwa serikali ya Saudi Arabia.
Msikiti huo ndipo alipozikwa Mtume Muhammad  na Medina  ni mji wa pili kwa utakatifu baada ya Mecca katika dini ya Kiislamu.
Mapema kulikuwa na shambulio la bomu katika mji wa mashariki wa Qatif.
Qatif  ni makazi ya  Waislamu wa madhehebu ya Shia na mlipuko huo unaonekana ulielekezwa katika msikiti wa Shia. Hakuna taarifa ya vifo wala majeruhi hadi sasa.
Aidha Mtu ambaye  anasadikiwa alikuwa anajitoa mhanga alijilipua karibu na ubalozi wa Marekani katika mji wa Jeddah wakati akishindana na wanausalama.Wanausalama wawili walijeruhiwa katika shambulio hilo.
Mitandao ya kijamii  kutoka Medina ilionesha  gari likiwaka moto na  maofisa wawili wa usalama wakiwa wamelala  karibu na gari hilo.
Aidha picha nyingine zilionesha  magari ya wagonjwa na polisi yakikimbilia eneo lililopo gari hilo lenye kuwaka moto.
Imeelezwa kuwa shambulio hilo limefanyika jioni wakati wa futari na inaonekana ililenga zaidi vikosi vya usalama.
Haijajulikana nani ameagiza mashambulio hayo.
Shambulio hilo limefanyika wakati mfungo wa ramadhani unafikia ukingoni na tayari watu wapo katika maandalizi ya Eid al-Fitr.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO