Meneja wa Mradi VSOMO  toka VETA kipawa  Gosbert Kakiziba (wapili toka kulia) akimuonyesha Ofisa Elimu wa mkoa wa Mbeya Charles Mwakalila (wakwanza kulia)  teknolojia ya masomo ya VETA kwa njia ya simu za Airtel wa VSOMO unavyofanya kazi wakati wa hafla ya kutambulisha kwa vijana huduma hii mkoani Mbeya katika chuo cha VETA mwishoni mwa wiki. Kutoka kushoto wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mauzo wa Airtel Mbeya Stratom Mushi na Mkuu wa chuo VETA Kipawa ambae ni  Msimamizi wa Mradi huo wa VSOMO Eng, Lucius Luteganya.


KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel wakishirikiana na VETA wametambulisha mfumo wa Masomo ya ufundi stadi yanayotolewa na VETA kwa njia ya simu za mkononi( Airtel VSOMO yaani VETA SOMO ) mkoani Mbeya mwishoni mwa wiki hii .
Mfumo huo tangu uzinduliwe Mei mwaka huu tayari umeandikisha vijana  zaidi ya elfu kumi ambao wanachagua kozi mbalimbali za VETA.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kutambulisha  mfumo wa Airtel VSOMO katika Ukumbi wa VETA Mbeya Mkuu wa Chuo cha Ufundi VETA Kipawa , Lucius Luteganya alisema:“Airtel na VETA tumeshafanya utambulisho kwa mikoa mingine minne ikiwemo Mwanza, Dodoma, Dar es salaam, Arusha na leo tuko Mbeya. mpaka sasa zaidi ya vijana  150  mkoani Mbeya wameshajiunga na mtandao wa VSOMO ili kuanza kusoma, hii inaonyesha kuwa mfumo huu wa kusoma kwa njia ya simu umekubalika hapa hata kabla hatujafika kuutambulisha”
“ninatoa wito kwenu vijana kujitoa na kuchangamkia FURSA hii inayoletwa kwenu na VETA kupitia mtandao wa Airtel ili muweze kujiajiri kupitia FURSA ya Airtel VSOMO”aliongeza Luteganya .
Kwa Upande wake Ofisa Elimu wa Mkoa wa Mbeya , Charles Mwakalila kwa niaba ya Mkuu wa mkoa huo  Amos Makalla alipongeza Mradi wa Airtel VSOMO na kubainisha kuwa mfumo huo ni Muarobaini wa kusaidia vijana wengi kupata elimu ya ufundi stadi hasa kipindi hiki  tunapoekea kwenye Uchumi wa Viwanda kama ulivyo mkakati ya serika ya Jamuhuri wa Muungano Tanzania
“Hii ni program nzuri sana tukiwa tunaelekea kwenye uchumi wa viwanda kama ulivyo mpango mkakati wa serikali, naamini tutahitaji watendaji wengi sana kwaajili ya viwanda hivyo wenye ujuzi kutoka VETA.  Nakumbuka hivi karibuni Naibu Waziri wa elimu  teknojia na Mafunzo ya Ufundi Eng, Stella Manyanya   alitoa tamko kwa mkuu wa VETA Mbeya, akisisitiza  VETA ihakikishe inasajili wanafunzi mara mbili ya waliopo,  hivyo kupitia mradi huu wa Airtel VSOMO wa  masomo ya VETA kwa njia ya simu  utasaidia sana  VETA Mbeya kusajili hata mara nne ya idadi iliyopo”
“naweza kusema Airtel VSOMO ni muarobaini wakupunguza changamoto ya ukosefu wa wataalam na watendaji wenye ujuzi tunapoelekea kwenye uchumi wa Viwanda” alisisitiza  Mwakalila
Naye mkuu wa Mauzo wa Airtel Mbeya  Straton Mushi alisema “Mradi wa Airtel VSOMO uko chini ya Airtel FURSA ili kuwasaidia vijana kujisomea kozi za ufundi  stadi kama vile ufundi wa pikipiki, ufundi simu, maswala urembo, ufundi wa kuchomelea na aluminium na kujipatia ajira papo kwa hapo,  Airtel tutahakikisha huduma hii inawafikia wengi kupitia mtandao wetu ulionea hapa nchini”
Airtel VSOMO nimfumo wa utoaji wa mafunzo ya Ufundi stadi kwa njia ya simu za mkononi uliobuniwa kwa ushirikiano kati Airtel na Mamlaka ya elimu na mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA)  hivyo kufanya simu ya mkononi kuwa Darasa.


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO