HUDUMA ya unywaji wa divai kwa mpango inatolewa mjini  Ottawa , Canada kwa lengo la kutibia walevi waliotopea.
Tiba hiyo inakwenda kinyume na  taratibu za kawaida  ambapo dawa ya ulevi wa kupindukia ni  kumuondoa kabisa  mlevi katika unywaji.
Kwa mujibu wa maelezo  utoaji huo wa divai hufanywa kwa  kiasi na mpangilio maalumu ambao umelenga kumbadili mhusika na  tabia ya ulevi uliokubuhu.
Tiba hiyo inatolewa katika nyumba ya Oaks ambayo awali ilikuwa hoteli na kubadilishwa kuwa nyumba ya huduma ya tiba kw awalevi waliotopea.
Aidha wengi wanaohudumiwa na hoteli hiyo ya zamani ni watu wa umri wa kati ambao wametopea katika pombe kiasi cha kuwaathiri.
Unywaji wa divai ambayo ina asilimia 13 ya kilevi huanza asubuhi kiasi cha saa moja na nusu ambapo wahusika hupewa kiasi cha mil200 na saa tatu na nusu usiku hupata mil140.
Mmoja wa wanaopata huduma hiyo Elisa Pewheoalook  amesema kwamba amefurahishwa na huduma hiyo kwani inamsaidia. Akiwa ametopea katika ulevi kwa takaribani miaka 40 anasema mtaani amekuwa akitumia kila anachokiona ili mradi apate nishai.
Akiwa anatokea Pond Inlet,  Kaskazini mwa Canada anasema si vibaya sana ukilinganisha na mtaani alikokuwa akitokea kwani alikuwa anakunywa dawa ya kusukutua mdomo na wakati mwingine dawa za kung’artisha nywele ili apate nishai.
Wahudumu wa hapo wamesema kwamba  yoyote anayeonekana kuwa na ulevi hapewi divai.
"haitokeo kila mara, lakini wakiwa wamekunywa sana, nawaomba waende vyumbani kulala," anasema  mmoja wa wafanyakazi wa nyumba hiyo , Lucia Ali ambaye ndiye anyeendesha baa.
Mpango huo ambao unajulikana kama Ottawa's Managed Alcohol Program - MAP – umetengenezwa kuweza kukabili changamoto za watu wasiokuwa na makazi ambao walikuwa walevi na wakashindwa kuacha kunywa kupindukia.
Mpango huo ni zao la wataalamu la miaka 15 iliyopita yenye lengo la kuwarejesha katika hali bora wananchi hao.
Lengo kuu ni kuhakikisha kwamba watu haow anatimiziwa changamoto zao ili watibike kw akupunguza kiwango cha pombe kila siku.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO