UFARANSA  kupitia ubalozi wake nchini imempongeza rais John Magufuli kwa kuhakikisha viashiria vya demokrasi vinaimarishwa kwa lengo la  kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wake.

Taifa hilo ambalo jana liliadhimisha  siku ya kitaifa ya Ufaransa maarufu kama Bastille Day , limesema vita ya Magufuli dhidi ya ufisadi na kutowajibika kwa utumishi wa umma ni moja ya uimarishaji wa demokrasia nchini.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Balozi wa Ufaransa nchini Melika Berak amesema kwamba taifa lake linatambua juhudi anazofanya Rais Magufuli katika kuhakikisha usalama waTanzania na  maendeleo.

Alisema juhudi za kuimarishwa taasisi za demokrasia kunakofanywa na rais Magufuli kunachochea maendeleo na uadilifu katika utumkishi wa umma.

Aidha alisema kwamba Ufaransa pamoja na kuheshimu juhudi za serikali ya Tanzania na kuahidi kuimarisha ushirikiano uliopo, balozi huyo pia alimshukuru rais Magufuli kw akutoa pole wakati taifa hilo lilipokabiliwa na shambulio kubwa la aina yake la ugaidi ambapo watu 130 waliokufa Novemba mwaka jana.

Alisema kauli ya rais magufuli alipofika ubalozini hapo inatia moyo na kuonesha ushirikiano wa kimataifa wa kukabili ugaidi kwa jaili ya kuleta usalama na amani.

Aidha alisema dunia inahitaji ushirikiano mkubwa wa kikanda kama inataka kujiimarisha na kuwa na maendeleo.

Aliisihi Tanzania kuendelea kuwapo katika jumuiya za kikanda kwa lengo la kukabiliana na chumi kubwa ambazo bila wao kushirikiana kikanda hawawezi kutopa ushindani unaotakiwa.

Akihutubia kwa lugha ya kifaransa huku akichanganya na Kiingereza kwa wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo mawaziri , mabalozi wa nchi mbalimbali na wananchi wa kawaida makao makuu ya ubalozi huo jijini Dar es salaam, Balozi Berak alisema taifa lake litaendelea kuchangia maendeleo ya Tanzania .

Alisema kwa mwaka jana ubalozi wake ulisaidia kufanikisha midahalo ya wazi inayogusa mazingira na mabaliliko ya tabia nchi, makongamano ya kiuchumi  na ushirikiano wa tasnia ya sanaa na kusema kwmaba mwaka huu itaimarisha maeneo hayo.

Katika sherehe hizo ambapo watu mbalimbali mashuhuri walikuwapo akiwamo waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim, waziri wa Madini na Nishati Profesa Sospeter Muhongo, Mwenyekiti Tume ya haki za binadamu, Serikali iliwasilishwa na Naibu Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Dk Suzan Kolimba.

Naibu waziri ambaye alimwakilisha Waziri wake Dk Augustine Mahiga, aliipongeza Ufaransa kwa siku yake hiyo ya kitaifa na kuahidi  ushirikiano wa Tanzania na Ufaransa kukuzwa zaidi.
Aidha alishukuru misaada ya Ufaransa kwa Tanzania hasa katika sekta ya miundombinu, kilimo na maji  na kuitaka jamii ya Tanzania kutumia ushirikiano uliopo wa kiserikali kutanua wigo katika uwekezaji.
Aliitaka jamii ya Watanzania kutumia jukwaa lililopo la ushirikiano kati ya Tanzania na  Ufaransa kartika biashara na viwanda kupata mapatna ambaow atashirikiano nao kufanikisha taifa hili kuwa la uchumi wa viwanda kwa kutumia raslimali zilizopo hapa nchini.
Katika historia Bastille ni ngome ya zamani  ambayo ni gereza iliyopo mjini paris. Watu wengi wa Ufaransa wanahusisha ngome hii na utawala wa kikatili wa falme ya Bourbon katika miaka ya mwishoni ya 1700.
Julai 14, 1789, vikosi vilivyoasi vilivamia Bastille ukawa ndio mwanzo wa mapinduzi ya Ufaransa,na  Julai 14, 1790 kukawepo na makubaliano yaliyowezesha kuanzishwa kwa utawala wa kifalme wa kikatiba.
Mwanasiasa Benjamin Raspail ndiye aliyependekeza Julai 14 kuwa mapumziko nchini Ufaransa, sheria ilipitishwa Julai 6,1880 na kuanzia Julai 14 Bastille Day ikawa siku ya mapumziko.
Alama muhimu za siku hiyo ni pamoja na mnara wa Eiffel uliopo Paris  na bendera ya taifa la Ufaransa.
mwisho

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO