MJI mmoja katika jimbo la Marekani la South Carolina umepiga marufuku  uvaaji wa suruali chini ya kiuno (KK) na kwamba mtu ambaye atakutwa na kosa hilo atalimwa faini ya dola za Marekani 600.

Mji wa Timmonsville,wenye wakazi 2,000wamepitisha sheria hiyo Jumanne wiki hii.

Imeelezwa kuwa ukikamatwa kwa mara ya kwanza unaweza kupewa karipio, la pili unaandikiw aonyo na  mara ya tatu utaliwa faini kati ya dola 100 hadi 600.

Amri za namna hiyo pia zimeshawahi kutolewa na miji ya Florida na Louisiana.

Mmoja wa madiwani amesema kwamba amri hiyo inaweza kuzua utata wa kibaguzi.

Hata hivyo mwaka  2007, ofisa mmoja wa Delcambre, Louisiana amesema kuzuiwa kwa mtindo huo wa uvaaji hauna uhusiano  ubaguzi.

Mtindo huo wa uvaaji ambao ‘una abudiwa’ sana na wasanii wa muziki wa hip-hop.

Imeelezwa katika tangazo  la Timmonsville kwenye gazeti la Florence kwamba itakuwa ni marufuku kwa mtu au kundi la watu  kuendesha au kutembea katika mitaa na barabara za Timmonsville  wakiwa watupu (uchi),kuonesha utupu au picha za kungonoana, au kuonesha makalio kw akutoyavika wakati wa kutembea au kusimama katika mitaa ya miji.

Aidha tangazo hilo limesema kwamba haikubaliki kuvaa suruali au kaptula kwa namna ambayo inaonesha nguo ya ndani kwa watu.

Meya wa Timmonsville, William James Jr  amekaririwa na gazeti la Florence akisema kwamba watoto wadogo hufanya kile wanachoona na hivyo ni lazima kulinda watoto hao.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO