Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , John Mongella akimpatia vipeperushi mmoja wa kijana katika kijiwe cha Bodaboda mkoani Mwanza wakati alipokwenda kuzindua mpango mpya wa kupata masomo ya ufundi kupitia simu zao za mkononi yajulikanayo kama VSOMO yanayoletwa na VETA kwa kushirikiana na Airtel kwa wakazi wa Mwanza


MKUU wa Mkoa wa Mwanza , John Mongella  amepongeza  taasisi ya  Mafunzo ya ufundi VETA na kampuni ya simu ya Airtel kwa kuvbuni mpango utakaowawezesha vijana kupata masomo ya ufundi kwa njia ya simu (VSOMO).
Alisema: “Mpango huu ni wakibunifu na umekuja wakati muafaka kwani utawawezesha vijana kupata masomo ya kiufundi ambayo yachochea kukua kwa uchumi wao.”
Pamoja na kuwasifia kwa hatua hiyo ameziomba taasisi hizo za VETA na Airtel  kuhakikisha kuwa VSOMO inaendelea kuwa mpango bora utakaosaidia watanzania kupata vijana wengi wenye taaluma kwa ajili ya kuendesha uchumi wa viwanda na kunufaika na ajira zitakazotokana na kufanya vizuri kwa viwanda hivyo.
Mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza aliwataka vijana wa mkoa huo kutumia fursa hii kwa kujiunga na masomo ya VETA kupitia VSOMO.
 “ Tunafurahi kwa Mwanza kuwa kati ya mikoa iliyopata nafasi ya kushuhudia uzinduzi huu kati ya VETA na Airtel. Nawapongeza kwa kushirikiana na serikali katika kuhakikisha tunawawezesha watanzania kupata elimu bora na ujuzi zaidi  kupitia VSOMO.” alisema Mkuu wa mkoa.
Kwa upande wake, Meneja huduma kwa jamii wa Airtel , Hawa Bayumi alisema   katika kutekelea za huduma kwa jamii , Airtel imedhamiria kuwawezesha na kuwaendeleza vijana kujikwamua kiuchumi kupitia programu mbalimbali ikiwamo ya VSOMO.
Akizungumza kuhusu VSOMO,  Mkuu wa chuo cha VETA kipawa , Lucius Luteganya, alisema kuanzishwa kwa mfumo wa VSOMO kutachochea mabadiliko makubwa yatakayotoa nafasi kwa watanzania kutumia mpango huo wa kipekee kupata mafunzo ya ufundi kwa urahisi na kwa gharama nafuu mahali popote kwa kutumia simu zao.
“Huu ni mpango wa kipekee Afrika mashariki na kati kwa kuwa hakuna taarifa zinazoonyesha mfumo kama kuna application yenye kutoa  mafunzo ya ufundi duniani. Wazi kabisa kukua kwa uchumi wa viwanda kutazidi kutokana na upatikanaji wa elimu za ufundi kwa uhakika na urahisi” alisema Luteganya.
Kozi vinazotolea kupitia application ya VSOMO  kwa sasa ni pamoja misingi ya ufundi wa pikipiki, kuweka umeme, ufundi wa simu, kuchomelea na kuunda vyuma na urembo.
Kozi hizi zinatolewa kwa gharama ya shilingi 120,000, muda wa kufanya mafunzo ya vitendo baada ya kufaulu masomo kwa njia ya mtandao ni saa 60. Hii inamaanisha kwamba aliyedhamiria kushona mathalani itamchukua mwenzi moja kumaliza masomo yake kupitia VSOMO.
mwisho

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO