Vijana wameaswa kuacha kukaa majumbani na kusubiri fursa za maendeleo ziwafate walipo na badala yake watumie muda mwingi kujishughulisha kwa kufuata fursa zilipo ili kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana nchini.
Akizungumza hayo wakati wa uzinduzi wa Kitabu cha taarifa ya utafiti wa Sauti za Vijana Tanzania Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana ,Ajira na walemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa vijana wasikae majumbani na vijiweni kutegemea Serikali iwapelekee fursa hizo.
“Vijana tusikae majumbani na kushinda vijiweni tukitegemea kwamba tutawaletea fursa huko mlipo , mnatakiwa mtoke na mtumie muda wenu kufikiri jinsi ya kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira kwa kutumia fursa zitolewazo” alisema Mhe. Mhagama.
Aidha Mhe. Jenista alisema kuwa  Serikali imeanza kutenga Shilingi Bilioni 15 kila bajeti kwa ajili ya kukuza ujuzi na kujikwamua kiuchumi ili kuleta maendeleo kwa vijana na taifa kwa ujumla.
Mbali na hayo Mhe. Mhagama aliunga mkono kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwamba ni marufuku kwa kumbi za starehe na mahali popote kuuza kilevi aina ya shisha kwani kinaharibu nguvu kazi ya vijana wa leo.
“Nasisitiza tena marufuku kwa  kumbi za starehe na mahali popote kuuza kilevi aina ya shisha kwani inaharibu uwezo wa kufikiri kwa vijana na kushindwa kufanya kazi matokeo yake uchumi wa nchi unazorota ,kwa yeyote atayekiuka maagizo haya hatua kali zitachukuliwa juu yake.
Aidha Mhe. Jenista aliwataka vijana kutumia vizuri fursa iliyotolewa na Serikali ya awamu ya tano kwa kutoa Shilingi Milioni 50 kwa kila kijiji ili kuleta chachu ya maendeleo kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Source: Ally Daud-Maelezo

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO