Wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anasema kwamba kwa ujumla hali ya nchi ni shwari pamoja na mauaji yaliyotokea Tanga, Geita, Mwanza , Mara na Dar es salaam, wanahabari wametakiwa kutumia kalamu zao kudumisha amani.
Akitoa hoja ya kuahirishwa Bunge jana waziri Mkuu alisema kwamba ni vyema wanahabari wakatumia kalamu zao kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuendelea kuifanya Tanzania kuwa kisiwa cha amani.
Alisema kwamba si vyema kuandika habari za kuleta hofu na uchochezi miongoni mwa jamii  kwani hali hiyo itakwimisha maendeleo ya taifa.
Alisema ni dhahiri kuwa matukio ya mauaji ya raia wasio na hatia hayakubaliki na kwamba ni wajibu wa vyombo vya habari kuendelea kuelimisha jamii.
Akizungumzia mauaji hayo yakiwemo yaliyotokea Ibanda Relini mtaa wa Utemini katika msikiti wa Masjid Rahman mkoani Mwanza, Super market ya Central Bakery mtaa wa swahili jijini Tanga na  Kibatini kata ya Chumbageni Tanga, Waziri Mkuu aseliama vyombo vya ulinzi na usalama  vimefanikiwa kuwakamata baadhi ya watuhumiwa na wengine kuuawa katika mapambano ya kurushiana risasi.
Alisema kwamba wanaendelea kuwaska awahusika ili wafikishwe katika vyombo vya sheria na kusema kwamba matendo ya kinyama hayatavumiliwa.
Hata hivyo amewakumbusha wabunge na wananchi wa Tanzania jukumu la ulinzi na usalama wa nchi yetu ni la kila tu kwa mujibu wa Katiba na hivyo wananchi wanawajibu wa kuzuia uvunjifu wa amani na uhalifu mahaliw anapoishi au kufanyia kazi.
"Naomba waheshimiwa wabunge, wanasiasa wote na viongozi wa madhehebu ya dini kutumia majukwaa ya siasa, mikutano ya dini na makongamano kusisitiza  umoja wa kitaifa na hivyo kuungana na serikali katika mapambano dhidi ya uhalifu unajitokeza" alisema.
Asubuhi wakati wa utoaji wa taarifa ya serikali kabla ya waziri Mkuu kuhutubia kuahirisha Bunge, Waziri wa Mambo ya ndani Mwiguku Nchemba akitoa  taarifa ya serikali ya Mauaji ya Rufiji  alisema kwamba kikosi maalum kimepelekwa  ili kushirikiana na  wapelelezi wa  mkoa w Pwani kuwaska waliohusika na mauaji hayo.
Alisema kwamba  watu wawili Mayonga na  Hamisi walikufa katika shambulio la kijambazi moja kwa risasi ya moto na mwingine kwa mapanga.
Ujambazi huo ulifanyika juzi saa moja na nusu katika eneo la Nyamwege.
kuhusu ugonjwa usiojulikana katika mkoa wa Dodoma waziri Mkuu amewataka watendaji kuhakikisha matokeo ya sampuli zilizokusanywa yanapatikana mapema ili chanzo cha ugonjwa huo kijulikane.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO