MKUU wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego amewataka Wakuu wapya wa Wilaya kuhakikisha kuwa wanafanyakazi kwa umoja ili kuweza kumaliza changamoto zilizopo mkoani humo hasa wakizingatia uwepo wa uchumi wa gesi unaopelekea mkoa kukua kwa kasi kubwa.

Akizungumza wakati akiwaapisha wakuu hao wa wilaya katika ukumbi wa Boma alisema kuwa mkoa umejipanga vizuri kuhakikisha kuwa wanatoa ushirikiano wakutosha katika utendaji ili kuweza kufanikisha ukuaji wa uchumi wa Mkoa wa Mtwara.

Alisema kuwa uwajibikaji na umoja unaweza kutoa fursa inayoweza kuongeza kasi ya maendeleo katika mkoa hali ambayo itaongeza hamasa ya wananchi kujituma katika kujenga uchumi na kukuza pato la kaya mkoa na taifa kwa ujumla.

“Nendeni makafanye kazi nyie ni maafisa mnaopaswa kwenda ‘field’ fanyeni kazi na wananchi moja kwa moja acheni kukaa ofisini na kujifanya mabosi hamtaweza kuona urahisi wa kazi yenu..fanyeni kazi kwa kujituma ili kuongeza ufanisi utakaokwenda sambamba na kasi ya serikali ya awamu ya tano” alisema Dendego
Wakingea mara ya baada ya kuapishwa wakuu hao wa wilaya waisema kuwa wapo tayari kufanyakazi kwa ushirikiano baina ya wananchi na wataalaamu walioko katika maeneo yao ili kuhakikisha wanatekeleza vyema majukumu yao hivyo  kuhalakisha maendeleo kwa wananchi wanakwenda kuwangoza
Mkuu wa wiaya ya Masasi Mzee Selemani Mzee, alisema kuwa wananchi wa wiaya yake wampe ushirikian ii aweze kutekeeza vyema majukumu yake na kwamba yeye kwa upande wake amejipanga kjuhakikisha anashirikiananao katika kila jambo ili kuhakisha maendeleo
“Mimi nikiwa kama kiongzi mkuu wa serikai katika wilaya yangu nitahakikisha nawangoza vingozi na watendaji wote wanafanyakazi kama yalivyo majukumu yao na wanatatua kero za wananchi kwa wakati ili kundoa malalamiko ya wananchi yasiyo ya lazima” alisema mkuu huyo wa wilaya
Mkoa wa Mtwara unawakuu wa wilaya watano ambao wote ni wapya walioteuliwa hivi karibuni na  Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Magufuli, ambao ni Mzee Selemani Mzee Masasi) Aziza Mangosongo- Newala ,Jaokim Wangabo- Nanyumbu,Dkt Khatibu Kazungu- Mtwara na Sebastian Walyuba –Tandahimba.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO