Picha ya maktaba ikionesha tohara wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni tarafa ya Challa 2014
Wanaume 39,939  wamefanyiwa tohara  mkoani Rukwa  katika  kipindi cha  mwaka 2015 -16 .
Hayo yalielezwa  na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa , David Kilonzo  ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa , Zelothe Steven  wakati wa  kukabidhi Mwenge wa Uhuru  Katibu Tawala  wa Mkoa wa Katavi Paul Chagonja  kijijini  Mirumba , wilayani Mlele  hafla  iliyohudhuriwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda.
Kilonzo alieleza kuwa  katika kipindi cha 2015 – 16  mkoa  wa Rukwa  ulilenga  kuwafanyia tohara wanaume wapatao 32,084  ambapo hadi Juni 30 , mwaka huu wanaume  wapatao  39,939  ikiwa  ni sawa na asilimia 124 ,
Aliongeza kusema  kuwa  zoezi hilo  la tohara kwa  wanaume  inafanywa kwa msaada  mkubwa  kutoka  kwa  washirika wa maendeleo w Walter  Reed Program (WRP).
Mkoa  wa Rukwa ulizindua rasmi kampeni ya Tohara kwa wanaume mwaka 2014 katika hafla iliyofanyika Tarafa ya Challa Wilayani Nkasi.
Hata hivyo Kampeni ya tohara ilianza  tarehe 17 Machi 2014.
 Tohara kwa wanaume husaidia kupunguza uwezekano wa akinamama kupata kansa ya kizazi  pamoja na kusaidia  kuepusha uwezekano wa maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa wanaume kwa zaidi ya asilimia 50
 Mwenge  wa Uhuru  ulianza mbio zake  mkoani  Katavi  baada  ya  kumaliza mbio hizo  mkoani Rukwa  ambapo ulikimbizwa katika wilaya  tatu  zenye  halmashauri nne  ikiwemo Sumbawanga , Kalambo , Nkasi  na Manispaa ya Sumbawanga.Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO