WANAWAKE KIJIJI CHA KITANGA KUZALISHA BIDHAA 300 ZA MUHOGO

Baadhi ya bidhaa zinazozalishwa kutokana na unga wa muhogo. Hii ni kazi nzuri ya kikundi cha akinamama wa Kitanga Green Voices kati...



Baadhi ya bidhaa zinazozalishwa kutokana na unga wa muhogo. Hii ni kazi nzuri ya kikundi cha akinamama wa Kitanga Green Voices katika Kijiji cha Kitanga wilayani Kisarawe.
Mchanganyiko wa mihogo, maharagwe, mboga za majani na nyama. Ni chakula kizuri sana hiki chenye aina nyingi za vitamin, wanga na protini.

PENGINE unafahamu faida tatu au nne tu za muhogo ambazo ni kuutafuna mbichi, kuuchemsha au kuuchoma; unga wake kwa ajili ya lishe, majani yake kama mboga ya kisamvu na dawa pamoja na miti yake inapokauka kutumika kama kuni.
Inawezekana hujui kama maganda ya mihogo baada ya kumenywa ni chakula bora cha mifugo yakikaushwa au mabichi.
Siyo ajabu pia hufahamu kwamba muhogo ukitwangwa mbichi na kuchujwa, maji yake yake yanatoa wanga (starch) ambao hutumika kutengeneza dawa za madoa, gundi katika samani, rangi za awali za ukuta na sukari (sugar syrup) na pia ni lishe nzuri.

Lakini zao la muhogo ni zaidi ya linavyofikiriwa kwa sababu licha ya faida hizo chache, lakini pia linazalisha bidhaa zaidi ya 300 kama ambavyo akinamama wa Kijiji cha Kitanga, Kata ya Msimbu wilayani Kisarawe wameamua kufanya.
Akinamama hao kupitia kikundi chao cha Kisanga Green Voices mbali ya kuzalisha unga pamoja na chips, sasa wanatengeneza bidhaa lukuki zenye ubora kama chapati, maandazi, skonzi, biskuti, tambi, cassava chop, na nyinginezo nyingi.
Hatua hiyo imekuja baada ya kupatiwa mafunzo kupitia mradi wa Green Voices unaofadhiliwa na taasisi ya maendeleo ya wanawake wa Afrika inayojulikana kama Women for Africa Foundation, ambayo iko chini ya Makamu wa Rais mstaafu wa Hispania, María Teresa Fernández de la Vega.

Baadhi ya akinamama wa Kitanga Green Voices wakiwa wameushikilia muhogo pamoja na viongozi wa kijiji na Kata ya Msimbu wilayani Kisarawe.
Kijana akiwa amebeba muhogo baada ya kuchimba shambani.

Kuanzishwa kwa mradi huo wa kusindika muhogo pamoja na bidhaa zake kumeliokoa zao hilo ambalo licha ya kuwa na manufaa makubwa kwa jamii, lakini limekuwa likidorora hata katika soko la vyakula.
“Tangu tumeanzisha kikundi hiki miezi mitatu iliyopita hivi sasa muhogo hauwezi kuozea shambani na wananchi wanaona umuhimu wa zao hilo,” anasema Mama Abia Magembe, ambaye ni mratibu wa mradi huo.
Mama Magembe, ambaye yeyé pamoja na akinamama wengine tisa walipatiwa mafunzo nchini Hispania kwa nia ya kuanzisha shughuli za ujasiriamali unaoendana na utunzaji wa mazingira pamoja na kupambana na mabadiliko ya tabianchi, anasema kwamba zao la muhogo sasa limepata thamani kubwa kijijini hapo na wana uhakika wakulima wa wilaya ya Kisarawe wanaweza kugeukia miradi kama hiyo ili kuongeza mnyororo wa thamani.
Akinamama 10 wanaofanya miradi mbalimbali ya ujasirimali kupitia mradi wa Green Voices wanatoka mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Kigoma, Kilimanjaro, Pwani na Mwanza.
Silvera Mujuni, Ofisa Chakula na Lishe wa Wilaya ya Kisarawe, anasema kwamba wilaya hiyo ina fursa kubwa ya kusindika na kuchakata mazao mengi yatokanayo na muhogo kwa kuwa zao hilo ndilo kuu kwa chakula na biashara.
Anasema kwamba, ardhi katika vijijini vingi vya wilaya hiyo inastawisha muhogo kwa wingi, hivyo ikiwa wananchi watajizatiti na kujifunza namna ya kuchakata bidhaa za muhogo wanaweza kupata faida kubwa kiuchumi.
“Muhogo ndilo zao kuu katika maeneo mengi ya wilaya hii ambayo haiwezi kustawisha mazao mengine kama mahindi, hivyo ni vyema wananchi wakajifunza utengenezaji wa bidhaa mbalimbali zinazotokana na zao hilo,” anasema Bi. Silvera aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Wilaya hiyo na ambaye ndiye alikuwa akiwafundisha akinamama hao namna ya kutengeneza bidhaa mbalimbali.

Diwani wa Kata ya Msimbu, Amina Lilomo, akizungumza na akinamama wa kikundi cha Kitanga Green Voices wakati wa uzinduzi wa mradi huo katika Kijiji cha Kitanga hivi karibuni.
Mshiriki kiongozi wa Kitanga Green Voices Women Group, Mama Abia Magembe, akiwahamasisha wanawake wenzake katika uzinduzi huo.

Awali Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Wazir Yakoub Wazir, aliwataka akinamama hao wajipange wasajiliwe rasmi ili waweze kunufaika na mikopo inayotolewa na serikali na taasisi nyingine za binafsi.
“Ofisi yangu iko wazi wakati wote, mkitaka kwenda kusajiliwa wilayani hata leo niko tayari kuwasaidia, nawaombeni mje niwasaidie hata namna ya kuandaa katiba ya kikundi pamoja na taratibu nyingine,” alisema.
Naye Diwani wa Kata ya Msimbu, Anna Lilomo, amesema atajitahidi – kwa kushirikiana na diwani mwenzake wa viti maalum Mossy Sultan Kufurumbaya – kuwapigania akinamama hao kwenye vikao vya Baraza la Madiwani ili waweze kupatiwa misaada na mikopo hata kupitia katika asilimia 10 ya bajeti ya halmashauri ambayo hulenga kuwasaidia wanawake na vijana.
“Bahati nzuri sisi hapa ni madiwani wanawake, kwa hiyo tutalipeleka suala la akinamama hawa kwenye Baraza la Madiwani na kuelezea umuhimu wa kuongeza thamani kwenye zao letu la muhogo ili limkomboe mkulima,” alisema Diwani Lilomo.
Mratibu wa Mradi wa Green Voices nchini Tanzania, Bi. Secelela Balisidya, anasema kwamba anafarijika anapoona wanawake wakihamasika kushiriki shughuli za maendeleo, hasa ujasiriamali unaolenga kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
“Suala la kuhakikisha uhakika wa chakula, kutokomeza umaskini, kuwawezesha wanawake kiuchumi na mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi ni mambo yaliyopewa kipaumbele katika Malengo Endelevu ya Dunia, hivyo wanawake wanaotekeleza miradi ya Green Voices wanayatekeleza malengo hayo kwa wakati mmoja,” anasema Secelela.

Diwani wa Kata ya Msimbu wilayani Kisarawe, Amina Lilomo (kushoto) na Diwani wa Viti Maalum, Mossy Sultan Kufurumbaya, wakiwa makini kusikiliza maelezo kuhusu namna ya kusindika bidhaa mbalimbali kutokana na zao la muhogo.
Akinamama wa Kitanga Green Voices wakiwa katika picha ya pamoja na mwandishi Tukuswiga Mwaisumbe (kilemba cha njano).

Muhogo ni zao linalochukuliwa na wengi kama la ziada hasa kwenye ukame, lakini wengi hulifanya kama mlo wa hamu bila kutambua kwamba zao hilo lina manufaa makubwa kwa lishe na kibiashara.
Wengi wanauchukulia muhogo kama chakula cha maskini, hawa wale wanaojitiahidi kulima zao hilo, huyapa kipaumbele mazao mengine kuliko muhogo.
Lakini muhogo ni zao mojawapo ambalo linaweza kuiepusha jamii na baa la njaa huku katika baadhi ya mataifa likitumika kama chanzo cha nishati ili kukabiliana na bei ya mafuta na nishati nyinginezo.
Baa la njaa ni tatizo kubwa linalozikumba nchi nyingi barani Afrika, Tanzania ikiwa miongoni mwazo, lakini licha ya watu kuhimizwa kulima muhogo, bado wanalipuuza zao hilo na kuliona kama zao fulani la mizizi tu.
Katika mikoa kama Lindi na Mtwara ambayo kwa miaka mingi inalima kwa wingi muhogo, chakula chao kikuu kilikuwa ugali wa muhogo.
Licha ya kudharauliwa kwa zao hilo, lakini siyo ajabu ukakuta mlo wa siku hiyo umetokana na muhogo kasoro chumvi na nazi, kwani inawezekana kuni zilizopikia ni matawi ya muhogo, ugali wa muhogo na kisamvu cha muhogo!
Na wakulima wengi katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara wanakula ugali wa muhogo pale wanapokosa unga wa mahindi, ambapo wanaokula ugali huo wa muhogo (Wazaramo wanasema ‘bada’ na Wamakua wanauita ‘matamba’) huonekana maskini wa kutupa.
Leo hii wanapohamasishwa kulima muhogo kwa sababu ya kustahimili ukame, bado wengi wanasuasua, lakini watakapoambiwa kwamba unga wa muhogo unatoa bidhaa nyingi zenye faida kubwa, huenda wengi wakaligeukia zao hilo na kulima kibiashara.
Inafurahisha sana siku hizi kuona watu wengi wakikimbilia ugali wa muhogo hata hotelini, lakini hiyo bado haijatosha kulirasimisha zao hilo ili liwe na tija kubwa.
Akinamama wa Kijiji cha Kitanga wanaweza kuwa mabalozi wazuri wa zao hilo, kwa sababu tayari wameanza kutengeneza bidhaa mbalimbali ambazo hata wananchi wa kijiji hicho wameshangazwa nazo baada ya kuzionja na kuona ubora wake.
Kilimo cha muhogo siyo tu kitasaidia kukuza pato la mkulima, lakini kinaweza pia kuokoa mazingira pamoja na kuisaidia Tanzania kuokoa karibu Dola za Marekani 20 milioni sawa na Shs. 42 bilioni zinazotumika kuagiza chakula nje, jukumu ambalo kikundi cha Kitanga Green Voices kimeamua kulibeba.

Mashine hizi ndizo zinazotumika kuuponda muhogo na kuucharanga kama chips. Kila kijiji kikiwa nazo kinaweza kutengeneza unga bora wa muhogo ambao utazalisha bidhaa mbalimbali.
Mihogo ikiwa imeandaliwa tayari kwa kuchakatwa kwenye mashine. 



Faida za muhogo ni nyingi kama zilivyoelezwa hapo juu, lakini kwa msisitizo ni kwamba, unga wake hutumika kutengeneza vyakula mbalimbali, baadhi ni uji na ugali, vitafunwa kama keki, mikate, skonzi, biskuiti, mandazi, mafuta ya lishe, sabuni ya unga, kuni, mboga, huksi pamoja na bidhaa nyingine nyingi
Mazao yanayopatikana katika mzizi wenyewe, miti na majani huweza kuzalisha bidhaa anuwai za viwandani kama vifaa vya nguo, karatasi, mafuta, kilevi, dawa za binadamu na plastiki wakati ambapo wanga hutumika kutengeneza dawa za madoa, gundi katika samani, rangi za awali za ukuta na sukari (sugar syrup).
Takwimu za kilimo cha muhogo duniani zinaonyesha kuwa, Afrika ni bara la tatu duniani kwa kuzalisha zaidi muhogo ambapo huzalishaji takriban tani milioni 102.6 kila mwaka.
Tanzania ni nchi ya nne kati ya wazalishaji wakubwa wa muhogo barani Afrika baada ya Nigeria, Ghana na Kongo DRC ambapo inaelezwa kwamba karibu ekari 670,000 za ardhi ya kilimo zinatumika kuzalisha muhogo, zao linalochangia karibu asilimia 15 za chakula kwa nchi nzima ambapo karibu kaya 1,213,958 huzalisha muhogo nchini.
Mikoa inayozalisha muhogo kwa wingi ni Mwanza, Mtwara, Lindi, Shinyanga, Tanga, Ruvuma, Mara, Kigoma, Pwani na maeneo yote ya Zanzibar. Ukanda wa Ziwa ni wazalishaji wakubwa zaidi ikifuatiwa na ukanda wa kusini. Mkoa wa Ruvuma huzalisha kati ya 5-10% ya uzalishaji wote Tanzania. 
Muhogo ndilo zao la pili kwa kuchangia pato la taifa kwa asilimia 19 baada ya  mahindi.
Taarifa ya Shirika la Utafiti wa Viwanda na Maendeleo ya Mazao ya Chakula Tanzania (TIRDO) inaonyesha kuwa zao la muhogo linastawi kirahisi.
Hii ni pamoja na kuvumilia ukame na halishambuliwi na magonjwa au wadudu wanaoathiri mazao mengine na pia muhogo unaweza kutoa mazao mengi katika ardhi duni ambayo mazao kama mahindi hayawezi kustawi.
Kwa mujibu wa TIRDO, muhogo ni zao la pili kuwa na wanga mwingi baada ya viazi vitamu ambavyo vina asilimia 20 hadi 30 ya wanga na kwamba asilimia 84 ya zao hilo hutumika kama chakula cha binadamu.

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,301,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4810,habari. dodoma,23,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: WANAWAKE KIJIJI CHA KITANGA KUZALISHA BIDHAA 300 ZA MUHOGO
WANAWAKE KIJIJI CHA KITANGA KUZALISHA BIDHAA 300 ZA MUHOGO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgzDTGvSzPbShRRJwA5UUERZwjotNTe_dsUKrIAR0_ciQOwCsG73u99R3nIrGOsfqIJIq227HnlW4DZrQds5MSKuRKRwsj6BKZUiK-wVt89SLviwLxbS6Wu7bq1hYRH2-HmArIiOTr6k-yZ/s640/Kitanga+9.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgzDTGvSzPbShRRJwA5UUERZwjotNTe_dsUKrIAR0_ciQOwCsG73u99R3nIrGOsfqIJIq227HnlW4DZrQds5MSKuRKRwsj6BKZUiK-wVt89SLviwLxbS6Wu7bq1hYRH2-HmArIiOTr6k-yZ/s72-c/Kitanga+9.jpg
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2016/07/wanawake-kijiji-cha-kitanga-kuzalisha.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2016/07/wanawake-kijiji-cha-kitanga-kuzalisha.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy