Kampeni za kuwania Ikulu ya Zambia zimeingia dosari jana wakati walinzi wa chama cha UPND  walipofyatua risasi kupinga  kuzuiwa kwa mkutano wao na jeshi la Polisi eneo la Kamwala.
Imeelezwa kuwa juhudi za Polisi kuzuia maandamano hayo zilijibiwa na milio ya risasi kutoka kwa walinzi wa UPND na kuwafanya polisi nao kujibu kujihami.
Imeelezwa kuwa maandamanao hayo yalishazuiwa na  polisi kwa sababu za kiusalama.
Imeelezwa kuwa katika piga nikupige mwanamke mmoja aliuawa.
Imeelezwa kuwa wakati polisi walipofyatua mabomu ya machozi kutawanya wafuasi wa chama hicho, walijibiwa na milipuko ya risasi na kuwafanya polisi kurejea nyuma na kisha kujibu mapigo kwa risasi za moto.
Baada ya hapo ikawa ni hekaheka za Polisi na wafuasi hao katika maizngira ambayo mmoja wa makada wa upinzani Lusaka Kamwala kusema ni kama uwanja wa vita.
Imeelezwa kuwa eneo la biashara la Lusaka la Central Business District lilivurugwa na vurumai hizi ambapo maduka na mabenki yalifungwa.
Baada ya mapigano hayo baadae maofisa usalama hao wa “UPND Security” walionekana wakikimbilia ofisi zao zilizopo Rhodespark.
Imeelezwa kuwa hali ya usalama imerejea tena na taarifa zaidi zitatolewa na polisi baadae.
Polisi wakishirikiana na Tume ya Uchaguzi  ya Zambia (ECZ) walishauri mkutano wa Chawama uahirishwe kwa hofu ya kutokea vurugu . lakini UPND wadharau amari ya Polisi na kuendelea mkutano wao.
Zambia itafanya uchaguzi wake Agosti 11 mwaka huu

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO