UMOJA wa Mataifa umesema kwamba 250,000 katika jimbo la Borno nchini Nigeria wapo katika hali mbaya kutokana na ukosefu nwa chakula na kwamba maelfu watakufa kama wasipopatiw amsaada haraka.
Jimbo hilo la Nigeria awali lilikuwa likidhibitiwa na kundi la Boko haram.
Shirika la Kuhudumia watoto la UNICEF limesema kwamba maeneo ambayo yanayodhibitiwa na  Boko Haram  hayana maji , chakula wala usafi.
Mwezi uliopita taasisi moja ya misaada imesema kwamba  watu waliokimbia kundi la Bokoharam wamejikuta wakikosa chakula hadi wanakufa.
Kundi hilo ambalo kw amiaka saba limeendesha harakati zake za uasi limesababisha watu elfu 20 kufa na zaidi ya milioni 2 kuwa wakimbizi nchini mwao.
Jeshi la Nigeria limekuwa likifanya kampeni kubwa ya kukabiliana na kundi hilo.
Unicef  imesema kwamba wakati maeneo mengi ya kaskazini mashariki ya Nigeria yanaaanza kufunguka tatizo kubwa la lishe kwa watoto linaanza kuonekana dhahiri.
Shirika hilo limesema kwamba watoto 244,000  wanakabiliwa na utapiamlo mkali na kwamba mtoto mmoja kati ya watoto watano atakufa kama asipopata msaada wa lishe mapema.
"Watoto 134 watakufa kila siku  kutokana na maradhi yanayosababsihwa na ukosefu wa lishe kama juhudi za kuwapeleka chakula hazitafanyika kwa haraka," anasema Manuel Fontaine,  Mkurugenzi wa Unicef kanda ya Afrika Magharibi na kati.
"Jumuiya ya kimataifa na wadau mbalimbali ni lazima washiriki katika kusaidia watoto hawa wasife kwa njaa. Hakuna nchi itakayoweza kurekebisha tatizo hili pekee peke yake"
Fontaine alisema ameona miji iliyoharibiwa ikiwa na watu ambao wana hali mbaya sana huku maelfu ya watoto wakiwa dhaifu zaidi wakihitaji msaada haraka sana.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO