Mama mlezi wa watoto wa kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira Hatarishi cha New Hope Family Group Kilichopo Mwasonga Kata ya Kisarawe 11, Kigamboni jijini Dar es Salaam, Asha Juma  akiwapa maelezo wafanyakazi wa  woolworths wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Joehans Mgimba (aliyeshika mtoto) juu ya kituo hicho wakati walipowapelekea msaada wa baiskeli na Vyakula mwishoni mwa wiki .


Mkurugenzi Mkuu wa maduka ya woolworths nchini, Joehans Mgimba akiwa amembeba mtoto Noline Gifti ,wakati walipokwenda kutoa msaada wa vyakula na baiskeli kwa watoto wa kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira Hatarishi cha New Hope Family Group Kilichopo Mwasonga Kata ya Kisarawe two, Kigamboni jijini Dar es Salaam.wengine kutoka kushoto niMkuu wa Operesheni ,Anna Grace Cussack na Mkuu wa Duka la Mikocheni Frank Ngoni.

Mkurugenzi Mkuu wa maduka ya woolworths nchini, Joehans Mgimba  (kushoto) na Mkuu wa Fedha Samson Katemi wakicheza na mtoto Noline  Gifti wa kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira Hatarishi cha New Hope Family Group Kilichopo Mwasonga Kata ya Kisarawe , Kigamboni jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mkuu wa Operesheni ,Anna Grace Cussack.


Mkurugenzi Mkuu wa maduka ya woolworths nchini ,Joehans Mgimba akisalimiana na mmoja wa watoto wa kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira Hatarishi cha New Hope Family Group, kilichopo Mwasonga Kata ya Kisarawe , Kigamboni jijini Dar es Salaam, wakati wafanyakazi wa Kampuni hiyo walipokwenda kutoa  msaada wa Beiskeli na Vyakula mbalimbali kituoni hapo.


Mkurugenzi Mkuu wa maduka ya woolworths nchini ,Joehans Mgimba akisalimiana na Majaliwa Anthony  wa kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira Hatarishi cha New Hope Family Group, kilichopo Mwasonga Kata ya Kisarawe , Kigamboni jijini Dar es Salaam, wakati wafanyakazi wa Kampuni hiyo walipokwenda kutoa  msaada wa baiskeli na vyakula mbalimbali kituoni hapo.Kulia ni mkuu wa fedha Samson Katemi.

Mkurugenzi Mkuu wa maduka ya woolworths nchini ,Joehans Mgimba akiwaasa  watoto wa wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira Hatarishi cha New Hope Family Group Kilichopo Mwasonga Kata ya Kisarawe , Kigamboni jijini Dar es Salaam, Kuzitunza baiskeli ambazo zitawasaidia katika usafiri wa kwenda shule .

Watoto wanaolelewa katika Kituo cha New Hope Family Group Kilichopo Mwasonga Kata ya Kisarawe , Kigamboni jijini Dar es Salaam, wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa maduka ya woolworths nchini ,Joehans Mgimba, wakati kampuni hiyo alipowapelekea msaada wa baiskeli pamoja na vyakula mbalimbali. Kulia ni mkuu wa fedha Samson Katemi.


Watoto wanaolelewa katika kituo cha Kulelea watoto waishio katika mazingira hatarishi cha New Hope Family Group Kilichopo Mwasonga Kata ya Kisarawe , Kigamboni jijini Dar es Salaamwakisukuma baiskeli pamoja na Wafanyakazi wa Woolworths wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Joehans Mgimba,mara baada ya kukabidhiwa msaada huo pamoja na vyakula na kampuni hiyo.


Watoto wanaolelewa katika kituo cha Kulelea watoto waishio katika mazingira hatarishi cha New Hope Family Group Kilichopo Mwasonga Kata ya Kisarawe , Kigamboni jijini Dar es Salaamwa wakiwa katika picha ya pamoja na  Wafanyakazi wa Woolworths, mara baada ya kukabidhiwa msaada wa baiskeli na vyakula mbalimbali.


Mkurugenzi Mkuu wa maduka ya Woolworths nchini, Joehans Mgimba akiwa amembeba kwenye baiskeli Majaliwa Anthony ,ambaye ni miongoni mwa Watoto wanaolelewa katika kituo cha Kulelea watoto waishio katika mazingira hatarishi cha New Hope Family Group Kilichopo Mwasonga Kata ya Kisarawe , Kigamboni jijini Dar es Salaam, ikiwa ni ishara ya kuonyesha jinsi watoto hao watakavyokuwa wanabebana wakati wa kwenda shule ili kuwahi masomo.kampuni hiyo ilitoa msaada wa baiskeli na vyakula mbalimbali kituoni hapo.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO