Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkingaakiwaaga Wazee katika kambi ya kulea wazee ya SukaMahela baada ya kutembelea na kuona hali halisi ya Mazingira katika kambi hiyo.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga amewataka watanzania hasa vijana wenye uwezo, wanaopekea na kukaa na wazee wao kwenye kambi za kulea wazee kuacha mara moja tabia hiyo.
Akiongea wakati alipotembelea kambi ya kulea ya wazee ya Sukamahela iliyopo Wilayani Manyoni Mkoani Singida Bi. Sihaba alisema kuwa     Serikali itaanza kuwachukulia hatua za kisheria watanzania wenye tabia hiyo kwani kufanya hivyo ni kukiuka sheria ya wenye ulemavu na wazee inayowataka wanafamilia kuwa na jukumu la kwanza la kumlea mzee na mtu mwenye ulemavu.
“Kumekuwa na utamaduni kwa baadhi ya vijana nchini kupeleka wazee kwenye hizi kambi za kulea wazee huku vijana hao wakionekana na kuwa na uwezo wa kuwalea, kwa kweli huu utaratibu sisi kama serikali hatuwezi kuuvumilia kwanza ni ukiukwaji wa sheria ya watu wenye ulemavu na wazee inayowataka wana familia kuwa na jukumu la kuwalea wazee, hivyo ni matarajio yetu kuwa kijana amlee mzee wake kama alivyolelewa yeye, Sisi kama serikali tutachukuwa jukumu la kuwalea wazee na watu wenye ulemavu wanaotoka kwenye familia zisizo na uwezo kabisa”. Alisema Bi. Sihaba.
Bi. Sihaba aliongeza kuwa utamaduni huo pia unawanyima fursa Wazee na watu wenye ulemavu wanaotoka kwenye familia zisizo na uwezo kupata huduma kutokana na baadhi ya watu kukwepa majukumu yao ya kifamilia wakati wanauwezo wa kufanya hivyo na kuzifanya kambi hizo kujaa na kushindwa kupokea watu wenye uhitaji.
Aidha, Bi. Sihaba alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano itaendelea kusimamia azma yake ya kuisaidia wazee na watu wenye ulemavu nchini ili kuhakikisha inapunguza na kuondoa kabisa changamoto zinazokabili kundi hilo.
Naye Afisa Mfawidhi wa Kambi hiyo Bw. Jeremiah Paul ameishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa kuzisimamia ipasavyo kambi hizi kwani itasaidia kuondoa kabisa changamoto zinazowakabili Wazee na watu wenye ulemavu katika maeneo hayo.
Akizungumza kuhusuutoaji huduma za Afya kwa Wazee wa Kambi hiyo Muuguzi wa Zahanati ya Serikali ya Sukamahela iliyokaribu na Kambi hiyo Bi Marry Sailale ameishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa kujenga zahanati hiyo karibu na kambi ya Wazee na kuomba kuongezewa vifaa na wafanyakazi katika zahanati hiyo ili kuongezea ufanisi katika kuwahudumia wazee wanaohitaji uangalizi wa karibu.
Source: Hassan Silayo-MAELEZO

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO