KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel kupitia huduma yake inayokuwa kwa kasi ya Airtel Money imeingia ubia na Benki ya NMB ili kutoa huduma kwa wakala wake wanaotoa huduma za Airtel Money kujipatia huduma ya salio na pesa taslim katika matawi ya benki hiyo popote nchini.
 
Akizungumza ubia huo, Mkurugenzi wa Airtel  Sunil Colaso alisema “tunachofanya Airtel na benki ya NMB ni mwendelezo wa mikakati tuliyojiwekea ya kuhakikisha tunaleta maendeleo katika huduma za kifedha nchini ili wateja wetu wapate huduma za uhakika na  nafuu. Pia kuwepo kwa sera bora za udhibiti na uwekezaji itachochea wawekezaji kuendelea kuboresha na kuweka miundombinu bora zaidi ya huduma ili kugusa mahitaji ya wateja wengi” alisema

Aidha alisema kwamba wanajisikia fahari kuona benki ya NMB inakuwa nguzo muhimu ya kutoa huduma za Airtel Money kwa kuwafikishia wakala salio kila walipo ili waweze kuhudumia wateja  kikamilifu.

Imeelezwa kuwa kwa ubia huo NMB itahudumia wakala  zaidi ya 45,000 ili kuweka na kutoa salio la Airtel Money wakati wowote katika matawi yao 160 nchi nzima.

NMB na Airtel inaingia Ubia kipindi ambacho Airtel Money pia imezindua kampeni yake kabambe ya Mr Money kwa lengo la kuwafikishia wateja wake taarifa za uhakika na unafuu katika huduma za Airtel Money.

 Airtel Money imefanikiwa pia kuleta huduma pekee za mikopo isiyokuwa na maharti magumu ya TIMIZA ambapo inawawezesha wateja na mawakala wake zaidi ya milioni 2 kujipatia mikopo kila wakati.

Mwisho.


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO