Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa ngumi za kulipwa unaotarajiwa kufanyika kesho katika uwanja wa ndani wa taifa.
Hayo yamesemwa na Rais wa Tanzania Proffesinal Boxing Organisation (TPBO) Yassin Abdalla (Ustaadh) wakati wa upimaji uzito wa mabondia chipukizi wanaotarajiwa kucheza mchezo huo kesho tarehe 21/08/2016.
Amesema kuwa pambano hilo ni pambano bora nchini kwani linashirikisha wachezaji chipukizi ambapo mshindi wa pambano hilo ataandaliwa pambano la kucheza kiwango cha kimataifa la shirikisho la ngumi duniani (WBF).
Aidha, amesema kuwa pambano hilo litafuata sheria na taratibu za mchezo wa ngumi za kulipwa hivyo kuwaasa mashabiki na mabondia kuwa na nidhamu wakati wa pambano ili kuepukana na vurugu.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya ngumi za kulipwa Tanzania Habibu Kinyogoli amewaasa marefa watakaochezesha mchezo huo kuwa waaminifu, kufuata Sheria na taratibu za mchezo wa ngumi za kulipwa ili kupata mshindi kihalali.
Kwa upande wake Promota wa mchezo wa masumbwi nchini na mdhamini wa pambano hilo Bw. Dotto Texas amesema kuwa wachezaji wake wamejiandaa kwa pambano hivyo ameomba mashabiki wa Mchezo wa Ngumi kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa ndani wa Taifa na kuwataka wachezaji hao kuwa na nidhamu ili kulipa heshima pambano hilo.
Wachezaji wanaotarajiwa kupambana kesho ni Jonase Segu mwenye uzito wa kilo 64.2 kutoka Magomeni Kagera pamoja na Mfaume Mfaume mwenye uzito wa kilo 64.0 kutoka Mabibo Jijini dare s salaam.
Source: Beatrice Lyimo-MAELEZO

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO