SHIRIKA la Polisi la Kimataifa (INTERPOL) lkimefanikiwa kumnasa kinara wa utapeli katika mitandao kutoka Nigeria aliyetambulika kwa jina moja tu Mike. Mtu huyo anasifa ya kutapeli kila mahali duniani.
Kinara huyo anadaiwa kuongoza watundu wengine 40 kuwaibia watu kwa njia ya intaneti zaidi ya dola  za marekani milioni 60.
Tapeli huyo anadaiwa kutumia njia tatuj kubwa. Ya kwanza ni kutuma virusi vinavyoingia katika mifumo na kuidhibiti,kudukua barua pepe za watu na pia kujifanya anashughulika na watu wanaohitaji wenza au mapenzi.
Imeelezwa kuwa kikosi maalumu cha kukabiliana na utapeli nchini Nigeria kilishiriki katika kukamatwa kwa kinara huyo.
"Katika moja ya shughuli yake alifanikiwa kumtapeli mtu dola za Marekani milioni 15.4," taarifa ya Interpol imesema.
"Mike" pia anadaiwa kuwa na netiweki ya utakatishaji wa fedha China ,Ulaya na Marekani.
Source:BBC

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO