Rais Jakaya Kiwete akiingia katika kituo cha afya Mgeta kukabidhiwa chumb cha upasuaji (picha zote za maktaba)

KITUO cha afya tarafa ya Mgeta, kilichopo Langali (lolo) ambacho Lions Club ilikabidhi chumba cha upasuaji kwa rais Jakaya Kikwete Agosti 2014 wakati alipotembelea tarafa ya Mgeta iliyopo wilayani Mvomero mkoani Morogoro kwa sasa hakina faida kwa wajawazito.
Pamoja na chumba hicho kutokuwa na faida kituo hiki kilichopo milimani na kutegemewa  na tarafa nzima yenye matatizo katika zahanati zake,pia kina matatizo lukuki ya huduma mbaya na ukosefu wa dawa hata za chanjo kwa watoto na kuwafanya wamama kurejea milimani bila huduma.
Aidha wale ambao wanafanikiwa kupata huduma hiyo huwa wamechelewa na kitu kidogo ni muhimu ili wafanikishe.
Kutokana na kutokuwepo kwa huduma muhimu za wajawazito, inapotokea changamoto kidogo mama mjamzitio na hata wagonjwa wa kawaida mgonjwa huambiwa watafute gari kwenda Morogoro huku kituo kina Landcruiser.


Na kama vile wanagawana na wenye magari, mtu analazimika kutumia takribani elfu 50 kumkimbiza mgonjwa wake hospitali ya mkoa kwa huduma.
Wanawake na wagonjwa wengine wameiambia Lukwangule kwamba wagonjwa wamepoteza hamu ya kutumia kituo hicho na kulazimika kufuta msaada kwa watu wanaoonekana kujua dawa kibaoni.
Wote wanaopata huduma Kibaoni kipraiveti wanasema kwamba daktari (?) anasikiliza na wanapata huduma safi.
Wanasema ukitaka kuona huduma kituoni ni lazima uwe na mchakato mfukoni au la utabaki hujui nani anakuja kukuhudumia.
Lukwangule ilipata bahati ya kutembelea hospitali hiyo Jumapili na kukiri kwamba labda serikali na wizara ya afya walishaamua kutoangalia cvituo vyao vya tiba vilivyopo katika milima ya Lukwangule upande wa Mgeta, Mungu awanusuru wajawazito hawa ambao wanatoka maeneo ya juu zaidi kusaka huduma na wanapofika wanaambia Morogoro ndiko kunakokufaa.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO