Ofisi za Bodi ya Mikopo zilizopo Mwenge, jijini Dar es Salaam zitakuwa wazi kwa siku mbili, Jumamosi, Agosti 6, 2016 na Jumapili, Agosti 7, 2016 kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 9:00 alasiri ili kutoa fursa muhimu kwa wadaiwa wote wa mikopo ya elimu ya juu ambao hawajaanza kurejesha mikopo kupata taarifa kuhusu madeni yao.

Bodi ya Mikopo imeshaanza kuwachukulia hatua wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu kwa kutangaza majina yao katika vyombo vya habari. Hatua zingine zitakazochukuliwa ni pamoja na:
i.              Kufikishwa mahakamani;
ii.             Kutozwa faini;
iii.            Kunyimwa fursa za kupata mikopo;
iv.           Kunyimwa fursa za masomo nje ya nchi; na
v.            Kuzuiwa kusafiri nje ya nchi.


Nyote mnakaribishwa ili kutumia fursa hii muhimu.

Imetolewa na:


Bw. Jerry Sabi,
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji,
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
S.L.P. 76068,
DAR ES SALAAM
Baruapepe: info@heslb.go.tz

‘Kuwa Mzalendo, Rejesha Mkopo wa Elimu ya Juu’

Ijumaa, Agosti 5, 2016

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO