Utamu wa muziki wa dansi wa kiafrika umegeuka kuwa pepo asiye sikia
ubani wala uvumba mbele ya washabiki wa muziki wa kiafrika kule ughaibuni,kwa takribani miaka 23 sasa Ngoma Africa band imekuwa katika medani ya muziki imefanikiwa kujizolea umaarufu kwa kuwanasa washabiki wa kimataifa katika kila kona. 

Urimbo wanaoutumia kuwanasa washabiki wao ni "Muziki wa dansi" au Bongo dansi kutoka uswahilini na jirani mwa afrika mashariki. bendi hiyo mashuhuri iliyoanzishwa mwaka 1993 na kiongozi wake mwanamuziki  mtanzania Ebrahim Makunja kwa majina ya usanii Kamanda Ras Makunja mkuu wa viumbe wa ajabu Anunnaki Aliens, bendi ya Ngoma Africa band na muziki wake imegeuka kuwa pepo aliyewaganda washabiki wa kila umri na kila jinsia.Kutokana na umahiri wake bendi hiyo imejiwekea historia ya  pekee ya kuwa bendi ya kiafrika katika majukwaa ya kimataifa yenye washabiki wengi.

Kikosi kazi cha Ngoma Africa band kinapokwea jukwaani kinakuwa na kazi moja tu hakuna kuremba remba bali kushambulia kwa muziki moto mpaka washabiki wanachanganyikiwa.
usikose kuwasikiliza at www.ngoma-africa.com 
jarida moja la ujerumani limeitaja bendi ya ngoma africa kuwa yenye mafanikio na imeshinda mapambano kwa kuwa bendi pekee ya kiarika kuteka soko la muziki ujerumani na ulaya som at http://www.afrikaportal.eu/portraet-ngoma-africa-band/

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO