TAASISI ya Uchunguzi wa Anga za Juu ya Marekani (NASA) imekamilisha zoezi lake la kwanza la mwaka mmoja kwa kundi la watu sita la kuishi katika upweke bila faragha ikiwa ni sehemu ya utafiti wa maandalizi ya safari ya kwenda kwenye sayari ya Mars.
Kundi hilo lilioanza maisha ya kiupweke Agosti 29 mwaka jana wakiishi bila hewa hewa ya kawaida wala chakula cha kawaida ndani ya dungu moja.
Wataalamu wanasema kwamba safari ya kwenda Mars huenda ikachukua kati ya mwaka mmoja na miaka mitatu.
Utafiti huo uliokuwa unafanywa na chuo kikuu cha Hawaii umeelezwa kuwa mrefu wa aina yake baada ya ule wa Urusi ambao ulichukua siku 520.

Baada ya kuishi katika mazingira hayo magumu kwa mwaka mzima, wahusika wamesema kwamba safari ya kwenda Mars inaweza kufanikiwa.
Mmoja wa wahusika kutoka Ufaransa,Cyprien Verseux, amesema kwamba anaamini safari katika siku za karibuni itawezekana kutokana na ukweli kuwa changamoto za kisaikolojia na kiteknolojia zitamalizwa.
Hata hivyo Mkuu wa misheni hiyo, Kamanda Carmel Johnston  amesema shughuli kubwa ilikuwa faragha kwa kuwa haikuwezekana kuwa na faragha.
Timu hiyo ilikuwa na Mfaransa ambaye alikuwa mtaalamu wa bayolojia,daktari wa Kijerumani na wamarekani wanne ambao walikuwa ni rubani, mjenzi, mwandishi wa habari na mtaalamu wa sayansi ya udongo.
Watu hao walitakiwa kuishi na vitu vichache sana na wakienda nje walikuwa wakitoka na vazi rasmi la anga za juu na kufanyakazi kwa lengo la kukwepa matatizo binafsi.
mwisho.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO