HUENDA wamarekani safari hii na dunia nzima wakapata mke wa Rais ambaye alishawahi kupiga picha za umodo akiwa mtupu na kutumiwa na majarida mbalimbali yenye hadhi Ulaya.
Gazeti la New York Post limeibua picha hizo za miaka 1990 zikionesha kwanini Trump anafikiria kwamba mkewe atakuwa festledi modo wa kwanza ndani ya Jumba jeupe la Marekani.
New York Post likisimulia kwa undani kwa lugha yake laini  limeandika kwamba miongo kadhaa kabla ya kuibuka katika mkutano wa uchaguzi wa Republican wa kumchagua mumewe kupeperusha bendera ya kuwania Urais mwaka huu, Bi. Trump, Melania Knauss  amepiga picha za utupu kwa jarida  la wanaume pekee la Ufaransa la Max.
Gazeti hilo likiandika limesema kwamba  binti huyo mzaliwa wa Slovenia ambaye ana miguu inayotamanisha akiwa na miaka 25 (sasa ana miaka 46 na mumewe 70) na akitambulika kwa jina la kazi yake kama Melania K.  alifanya kitu kilichowatoa jasho wanaume baada ya kupiga picha za utupu zilichukuliwa katika eneo la Manhattan mwaka 1995.
Aliyepiga picha hizo zenye mvuto wa kipekee ni  Mfaransa Alé de Basse¬ville.
Picha hizo ambazo zimetolewa pekee kwa sasa katika uorijino wake kwa gazeti la Post chapisho la Julai 31 zinaonesha akiwa mtupu katika pozi mbalimbali huku akikinga kwa mikono yake maeneo yake ya faragha. 
Alichokuwa amekivaa ni mchuchumio  na alifotolewa kwa mbele na kwa nyuma aidha kila upande.
“Melania  alikuwa bomba na alikuwa mkarimu sana kwangu,”  alisema de Basseville akizungumza na The Post, akiongeza kwamba binti huyo hakuona kinyaa wala aibu katika uchukuliwaji wa picha hizo.
Picha hizo za Melania za utupu zilichapishwa mwaka 1996 Januari katika jarida la wanaume pekee la Ufaransa la Max. Jarida hilo kwa sasa halipo limefungwa baada ya kufisilika mwaka 2006.
 “Nilistaajabishwa sana nilipoziona picha zile baada ya kusafishwa… zilikuwa tamu mno kuliko nilivyofikiria,”  alisema mtu wa ndani katika tasnia ya urimbwende ambaye alikuwapo wakati zikichukuliwa picha hizo.
“Lakini Melania alikuwa mtulivu katika shughuli nzima, alikuwa profesheno hasa.”
Kwa fikira zake  de Basseville,picha hizo kwa kimombo zilitoa sura kamili ya Renaissance and a celebration of the female body.
 “Nadhani ni muhimu kuonesha uzuri na uhuru wa mwanamke. Na ninajisikia vizuri sana kupiga picha hizi kwani zinashangilia uzuri wa Melania,”  alisema.
Wakati picha hizo zinachukuliwa Melania alikuwa ndio kwanza amerejea mjini New York kutoka katika shughuli za urimbwende huko Paris  Ufaransa na Milan italia.
Binti huyo ametokea sana katika matangazo ya kibiashara na kuna wakati alikuwa katika matangazo ya sigareti ya Camel.
Alipoulizwa kuhusu picha hizo Trump alilijibu gazeti la Post: “Melania alikuwa mmoja wa mamodo waliofanikiwa sana, alipiga picha nyingi za umodo ambazo zilisambaa katika majarida  makubwa . Hizi ni picha zilizopigwa kwa ajili ya jarida moja la Ulaya kabla sijamjua Melania. Katika bara la Ulaya picha kama hizi ni za kawaida na ni fasheni.”
Trump aliunganishwa na Melania mwaka 1998, kwenye hafla ya New York Fashion Week  katika klabu ya Kit Kat iliyoandaliwa na Paolo Zampolli, ambaye wakati huo alikuwa ndiye meneja wa Melania kupitia kampuni yake ya ID Model Management.
Wawili hao walioana mwaka 2005 katika hafla iliyofanyika katika makazi ya Trump ya Mar-a-Lago yaliyopo Palm Beach, Florida.
Mshauri wa masuala ya mawasiliano katika kampeni ya Trump, Jason Miller,  baadaye alimtetea mwanamama huyo na kusema kwamba hakuna ubaya kwani ni sanaa inayoshabikia mwili wa binadamu akisisitiza kwamba hakuna cha kufadhaika katika hilo kwani ni mwanamke mrembo.
Melania Trump (akiwa amezaliwa Melanija Knavs, Aprili 26, 1970 huko Novo Mesto; ambaye baadaye alilipa jina lake mfumo wa kijerumani Melania Knauss) ni mke wa tatu wa bilionea Donald Trump ambaye kwa sasa anawania kuingia Ikulu ya Marekani.
Ni mtu mwenye asili ya Slovenia akiwa  ni dizaina wa vito na saa. Aidha alikuwa modo.
Akiwa amezaliwa Slovenia ilikuwa sehemu ya taifa la Yugoslavia alipata ukazi wa kudumu Marekani mwaka 2001 na kuwa raia mwaka 2006.
Akiwa anaongea lugha tano  za Kislovenia, kiingereza, kifaransa,Kiserbia na Kijerumani alianza shughuli z aumodo akiwa na miaka 16 akiwa na miaka 17 alipozi kwa picha za fasheni za mpigapicha wa fasheni Stane Jerko.
Akiwa na miaka 18 alitia saini mkataba na kampuni ya mitindo ya Milan Italia na akawa wa pili katika shindano la muonekano bomba wa mwaka wa jarida la Jana Magazine la mwaka 1992 lililofanyika Ljubljana,.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO