UKWELI Kuhusu kutenguliwa kwa Mkurugenzi wa Bagamoyo na uhusiano wa kushindwa CCM katika majimbo ya Mlimba na Kilombero, mkoani Morogoro 2015

Taarifa kwa vyombo vya habari                                                        Agosti 1, 2016 Kuhusu kutenguliwa kwa Mkuruge...



Taarifa kwa vyombo vya habari
                                                       Agosti 1, 2016
Kuhusu kutenguliwa kwa Mkurugenzi wa Bagamoyo na uhusiano wa kushindwa
 CCM katika majimbo ya Mlimba na Kilombero, mkoani Morogoro 2015.
Julai 30, mwaka huu, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli alitengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Bagamoyo, Bibi Azimina A. Mbilinyi.  Taarifa hiyo iliyosainiwa na Eng. Musa Iyombe, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, ilisema Rais alitengua uteuzi huo kwa sababu hakuridhishwa na utendaji kazi wa Bibi Azimina A. Mbilinyi.
Baada ya taarifa hiyo, wapo watu wanaohusisha kutenguliwa mkurugenzi huyo na kushindwa kwa CCM katika majimbo ya Mlimba na Kilombero. Kabla ya kuhamishimiwa Bagamoyo, Bibi Mbilinyi alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilombero, yenye majimbo mawili ya uchaguzi, ambayo yote wabunge wake ni wa kambi ya Chadema; Peter Lijualikali-Kilombero na Suzan Kiwanga Mlimba.

NINACHOKIJUA KUHUSU MAJIMBO HAYA
Naandika haya kama mtu ambaye nilishiriki kura za maoni na niliona kasoro zilizotokea na ndizo zilizosababisha CCM kushindwa, unaweza kuona hata madiwani tumepata wachache kuliko wenzetu. Nilikuwa kati ya watia nia katika CCM Jimbo la Mlimba, wengine niliogombea nao ni Dk Frederick Sagamiko (ambaye sasa ni Mkurugenzi-Maswa), Senorina Kateule, Godwin Kunambi (ambaye ndiye alipitishwa na chama kugombea), Augustino Kusalika, George Swevetta, Castor Ligallama, Profesa Jumanne Mhoma, Fred Mwasakilale.
Kwa upande wa Jimbo la Kilombero watia nia walikuwa Kanali mstaafu Harun Kondo, Vitus Lipagila, Abdullah Lyana, Oscar Mazengo,  Japhet Mswaki, Paul Mfungahema, John Guninita, Abubakari Asenga (ambaye sasa ni katibu tawala Rombo) na Abdul Mteketa.

MCHAKATO WA KURA ZA MAONI
Katika mchakato wa kumpata mgombea wa Ubunge, hapo ndipo tatizo lilipoanzia; Kwa mfano katika Jimbo la Mlimba, tangu siku ya kwanza ya kampeni katika kumsaka mgombea, tukiwa tunatoka makao makuu ya wilaya (Ifakara), tulipofika hotelini kata ya Mlimba ugomvi uliibuka miongoni mwa watia nia.
Msingi wa ugomvi huo uliozaa uhasama, ilikuwa mmoja wa watia nia kumrushia maneno mwingine kiasi cha kutaka kupigana; sababu kubwa ni kwamba sote tuliwahi kufika katika kambi yaani hoteli ambayo tulitakiwa kuwepo kabla ya kwenda vijijini kwa wanaCCM wenzetu kujinadi, lakini kuna mtia nia ambaye alichelewa zaidi ya saa masaa matano kufika tulipotakiwa kuwepo yaani hapo kwenye kambi, kitendo ambacho kilitafsiriwa kama alikuwa anafanya kampeni.
Aidha mtia nia huyo aliambiwa na mtia nia mwenzake (huyo waliyekuwa wakigombana) kwamba yeye hakupaswa kugombea Jimbo la Mlimba, kwa sababu makazi yake ni kata ya Mkamba, ambayo iko katika Jimbo la Kilombero.
Kama hiyo haitoshi, katika kura za maoni kulikuwa na malalamiko kuwa baadhi ya watia nia ni kama walipandikiza watu, kwamba yuko mtia nia ambaye kulipokuwa na mkutano wa wana CCM ili kusikia sera za watia nia, aliposimama yeye alikuwa anashangiliwa sana, na wakati mwingine kama yeye alikuwa wa kwanza kuzungumza, basi baada ya yeye kuongea, wengi wa wana CCM walikuwa wakiondoka kwenye mikutano.

OFISI YA CCM WILAYA KUTOCHUKUA HATUA
Licha ya malalamiko hayo kuwasilishwa wilayani, hapakuwa na hatua za haraka zilizochukuliwa. Kitendo hiki kiliendelea kuimarisha ufa ndani ya CCM hasa miongoni mwa wagombea (watia nia).

KURA ZA MAONI NA BAADA YA MATOKEO
Baada ya kumaliza kujinadi, uchaguzi ulifanyika katika vituo mbalimbali huku tukiambiwa tuweke mawakala katika maeneo ya kupigia kura. Wengi tulifanya hivyo. Kwenye kura za maoni, miujiza ilianza kutokea, kwamba katika kata fulani, wakala wako anakwambia umepata kura kiasi fulani, wilayani tulikuwa tukiona kura tofauti. Wengi tulipohoji tuliambiwa tutulie kungekuwa na vikao kujadili kama kuna kasoro na namna gani twende sawa.

NINI KILITOKEA?
Hadi leo hakuna kikao kilichoitishwa na wilaya kujadili malalamiko ambayo watia nia waliyawasilisha wilayani. Matokeo yake ni nini? Ukweli ni kwamba wapo wanaCCM wengi walijitoa CCM moja kwa moja na kuungana na upinzani, huku wengine walifanya hivyo kwa siri, sababu kubwa ni kwamba waliona ofisi ya Wilaya haikuwatendea haki kwa kutofanya kikao, kitendo ambacho kilitafsiriwa kama walikuwa na mgombea wao waliyemtaka, japo ofisi ya CCM wilaya Kilombero imekuwa ikikanusha hilo.
Anguko la CCM katika Wilaya ya Kilombero lilitokana na dharau; baadhi ya viongozi kuamini kwamba wanaweza kwenda mbele hata kama watawadharau au watayadharau malalamiko ya watia nia wengine.

USHAHIDI WA HILI
Ni mimi, Dismas Lyassa pekee ndiye niliyeshiriki kwenye mikutano ya kuwanadi wagombea, niliwasha gari yangu kutoka Dar es Salaam hadi Ifakara kwenye kumnadi Abubakar Assenga. Wengine walikuwa na sababu zao zikiwamo kutofurahishwa na mchakato mzima wa upatikanaji wa wagombea.

INAWEZEKANAJE BIBI AZIMINA A. MBILINYI AKATENGULIWA HARAKA HIVI
BAADA YA KUHAMISHIWA BAGAMOYO?
Kama nilivyotangulia kusema, natoa taarifa hii kama mtu ambaye nayajua mazingira ya kushindwa kwa CCM yangu katika uchaguzi, mtu ambaye najua kwanini CCM tulishindwa mwaka 2015. Huenda wengine waliona tofauti lakini haya ni kwa namna ninavyoona mimi kama Dismas Lyassa.
Kwa bahati nzuri katiba inaruhusu kila mtu kutoa maoni yake katika jambo kwa kadri anavyoona yeye, ndivyo ninavyoona mimi kilichotokea kwenye uchaguzi 2015, wengine wanaweza kuwa na maoni tofauti, nao waheshimiwe kwa sababu kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni kwa kadri anavyoona yeye.
Katika mitandao ya kijamii, yuko mwanasiasa mmoja maarufu nchini anahusisha kuanguka CCM eti kwa sababu alishindwa kuisaidia CCM kushinda. Kwa mazingira niliyoyaeleza wagombea wetu wangewezaje kushinda? Mfano katika kijiji cha Mofu pekee, zaidi ya viongozi 15 wa matawi na taasisi mbalimbali walihama CCM na kwenda upinzani, jumatano ya kuelekea jumapili ya uchaguzi. CCM haijapoteza majimbo ya Mlimba na Kilombero pekee, kwa hiyo sioni mantiki ya kuhusisha haya ya Azimina na siasa.
Wapo wanaoweza kusema aaah sasa mbona Rais amechukua maamuzi saa chache baada ya CCM kushindwa kesi za kupinga matokeo….jambo humtokea mtu wakati wowote, iwe anatoka usingizini…kazini nk…mtu anaweza kufa hata kama anatoka nyumba ya ibada…huwezi kusema si angesubiri kwanza.

Bibi Azimina A. Mbilinyi
Akiwa Mkurugenzi Kilombero niliwahi kuwasiliana nae kwa simu/whatsap kuhusu kijana mmoja aliyesomeshwa na mjane. Kwamba, kijana huyo alipata ajira katika halmashauri hiyo kama afisa maendeleo, lakini aliporipoti akaambiwa arudi atatafutwa. Nilimpigia Azimini mara kadhaa kujua juu ya suala hili na majibu yalikuwa ni kwamba anafanyia kazi, huku kukiwa na utata wa kama nafasi hiyo ambayo ilikuwa ni kwa mujibu Tume ya Utumishi wa Umma kama ilikuwa bado au la.
Maana yake ni nini? Ikiwa mimi najua hili, je wewe ulikuwa unajua? Kumbe ni kwamba sio sahihi kuzungumza mambo tusiyoyajua. No research, no right to SPEAK. Huyo kijana ambaye amesomeshwa na mjane, hadi leo hana kazi, anaishi kwa mama yake kwenye nyumba moja inayotazamana na hoteli ya Landmark Ubungo, Dar es Salaam. Hana ajira, licha ya kwamba tayari alishaipata, ameambiwa asubiri, leo ni zaidi ya miezi nane tangu aambiwe asubiri, hakuna jibu lililonyooka.
Ambacho nataka umma ufahamu ni kwamba ukweli kuhusu majimbo ya Kilombero na Mlimba ni huo, kwamba wapo wana CCM walioshirikiana na vyama vya upinzani ili tu ishinde kwa sababu waliamini hawakutendewa haki na chama hasa pale kilipofunga milango ya kuwepo kwa mikutano ya suruhu.

NILIWAHI KUSHAWISHI WANACHAMA NA VIONGOZI WA CCM KUWAONDOA VIONGOZI WA WILAYA LAKINI NIKAOMBWA NIACHANE NA HILO ILI LISILETE ATHARI KWA CHAMA
Kama mtakumbuka baada ya uchaguzi mkuu, niliongoza mpango wa kufufua CCM Kilombero, niliwasiliana na viongozi wa kata zote, matawi na wanachama; azma ilikuwa kwanza ni kuwaondoa viongozi wa wilaya, hata hivyo nilishawishiwa na baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa chama kwamba suala hilo lingeweza kuharibu zaidi, kwa hiyo niwe na utulivu na nifanye mawasiliano na wote ambao nilishawasiliana nao ili kuahirisha chochote nilichokuwa nimekipanga.
Nilifanya hivyo, kutokana na kuwatii hasa baada ya kuelezwa njia nyinginezo ambazo zingeweza kuweka mambo sawa ndani ya chama.
Naomba ulimwengu ufahamu kwamba hayo ndiyo yaliyotokea katika majimbo ya Mlimba na Kilombero; shida kubwa ni sisi wenyewe tulishindwa kuungana baada ya kura za maoni, na viongozi hadi leo hawajatuunganisha.
Kwa kuanguka kwa CCM wa kuondolewa ni viongozi wote wakuu wa CCM Wilaya kutokana na sababu 1.Kushindwa kuwa na mkakati wa kuimarisha chama, hasa kutokana na ukweli kwamba hata wakati wa kura za maoni, wapo wanachama walitoa lawama za wazi kwamba viongozi wa wilaya wamekuwa wazito kutembelea kata na matawi ili kuyaimarisha. 2. Pia hawakuona umuhimu wa kuweka suruhu baina ya watia nia 3. Kuna haja ya viongozi wakuu wa chama chetu (CCM) kuomba kibali ili waingilie mawasiliano ya simu ya viongozi wa CCM Wilaya Kilombero, hasa laini za tigo na Airtel, kuanzia Julai 2015 hadi Oktoba 2015. Nafahamu ninachokiongea ndio maana sijataja laini za simu za makampuni mengine.


TUUNGANE KUIMARISHA NCHI
Kutangaza mambo tofauti ni kupotosha umma bila sababu, tuungane na Rais katika kuimarisha nchi. Miaka mingi tumekuwa tukililia Rais mchapakazi, sasa amepatikana ni vema kumtia moyo.
Kwani hujawahi kuwa na rafiki, halafu ukabini kwamba haikuwa sahihi kuwa nae?
Ni mambo ya kujitafakari badala ya kulaumu.
Tanzania kwanza; tuungane kuijenga nchi yetu.
Wako katika ujenzi wa taifa

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,302,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4816,habari. dodoma,24,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: UKWELI Kuhusu kutenguliwa kwa Mkurugenzi wa Bagamoyo na uhusiano wa kushindwa CCM katika majimbo ya Mlimba na Kilombero, mkoani Morogoro 2015
UKWELI Kuhusu kutenguliwa kwa Mkurugenzi wa Bagamoyo na uhusiano wa kushindwa CCM katika majimbo ya Mlimba na Kilombero, mkoani Morogoro 2015
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEho8d9II-V5U8azUBvqi4qrcVUdgsBNNAJdBoEzh35lJhO08_6sPZlj1gIM5QY8-OtLW2E0TIdCUKpLBZqYjRc6A_64inofULPjBfxm2MsifdHjCmCUXeMcauSebun4Dk4XlBcxWjgk9hI/s320/Dismas+Lyassa.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEho8d9II-V5U8azUBvqi4qrcVUdgsBNNAJdBoEzh35lJhO08_6sPZlj1gIM5QY8-OtLW2E0TIdCUKpLBZqYjRc6A_64inofULPjBfxm2MsifdHjCmCUXeMcauSebun4Dk4XlBcxWjgk9hI/s72-c/Dismas+Lyassa.jpg
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2016/08/ukweli-kuhusu-kutenguliwa-kwa.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2016/08/ukweli-kuhusu-kutenguliwa-kwa.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy