Wanawake zaidi wenye umri wa miaka 40 na kuendelea  ndio wanaongoza kwa kuzaa huku wale ambao ni  chini ya miaka 20 wakiwa wamepunguza kasi nchini Uingereza.
Takwimu hizo ni za England na Wales hazijawahi kutokea kwa kipindi cha miaka 70 .
Ofisi ya Takwimu ya Taifa zinaonesha kwamba kulikuwa na  uzazi wa watoto 697,852 kwa mwaka jana,2015 na kwamba kulikuwa na  uzazi wa 15.2 kwa kila wanawake 1000 walio na umri zaidi ya miaka 40 ukilinganisha na 14.5 kwa kila wanawake 1000 vijana.
Mara ya mwisho wanawake zaidi ya maika 40 waliongoza kwa uzazi ilikuwa ni mwaka 1947 wakati vita kuu ya pili inanukia.
Imeelezwa kuwa upataji mimba kw avija aumekuwa ukipungua kwa kasi kutoka uzazi 33 kwa kila vijana 1000 katika miaka ya 1990, huku ujauzito kwa wanawake walio na umri mkubwa  umeongezeka kutoka 5.3 kwa wanawake 1000 katika mwaka 1990.
Imeelezwa kuwa wastani wa umri wa kuwa na watoto sasa ni 30.3, takwimu ambayo imekuwa ikiongezeka kutoka mwaka 1975.
Imeelezwa kuwa kuwapo kwa utabibu wa uzazi na huku wanawake wengi wakiwa katika masomo ya juu zaidi na gharama za kuwa na watoto kndio sababu za watu kuzaa katika umri mkubwa.
Liz McLaren, mkuu wa takwimu muhimu amesema kwamba  mtiririko  wa wanawake wenye umri mkubwa kuwa na watoto imeendelea mwaka jana.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO