Meneja wa Tawi wa Airtel  Ausha Bi Monica Ernest akiwa na Mkuu wa mauzo wa Airtel kanda ya kaskazini Bw, Brighton Majwala Wakizungumza na  baadhi ya wajasiriamali na watoa huduma ya usafiri wa Boda boda Arusha eneo la stand kuu Arusha jinsi wanavyoweza kujiunga na mfumo wa VSOMO na kusoma masomo ya Ufundi stadi kupitia mtandao wa Airtel

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel na VETA imeingia mkoani Arusha kuendelea kutoa uelewa kwa vijana kukamata fursa na kusoma kozi mbalimbali za ufundi toka VETA kupitia mfumo wao wa simu ujulikanao kama VSOMO.
Zaidi ya vijana elfu kumi na nane nchini wamejisajili kusoma kwa mfumo huo wa simu za mkononi huku mikakati yao ikiwa ni kuongeza kozi 10 zaidi ili wanafunzi kuendelea kujisomea.
Mkuu wa mauzo wa kampuni ya simu kanda ya kaskazini   Brighton Majwala akizungumza na wajasiriamali na madereva bodaboda  waliokusanyika Stand kuu  Arusha  aliwataka vijana kuchangamkia fursa hizo ili kujiendeleza.
“Airtel na Mamlaka ya ufundi stadi VETA lengo letu ni kuwafikishia elimu ya ufundi vijana wengi nchini, upande wetu Airtel tunahakikisha mtandao upo vyema ili vijana waweze kusoma bila kukwama, hadi leo hii tayari vijana zaidi ya milioni 18 wameshakamata Fursa hii kwa kupakua aplikesheni au mfumo huu wa VSOMO katika simu zao” alieleza Majwala.
Majwala aliendelea kusema: “mpango wetu Airtel na VETA  kuongeza uelewa kwa  vijana ili wasome kozi zilizopo sasa ikiwemo ya  ufundi piki piki, umeme wa nyumbani, ufundi simu, ufundi wa aluminium, utaalam wa masuala ya urembo, pamoja na ufundi wa kuchomea vyuma”.
Naye  Meneja  Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema kutokana na VSOMO kuwa na idadi kubwa ya vijana waliojisajili  tayari Airtel kwa kushirikiana na VETA wako katika utekelezaji wa kuongeza kozi zingine zaidi ya kumi ili kuongeza wigo wa kuchagua pamoja
“Tunampango wa kuongeza kozi zingine 10 kabla ya mwezi wa 12 ambapo sasa hivi tayari VETA wako katika utaratibu wa kuzifanyia kazi kozi hizo ili ziweze kuingia katika mtandao” alisema Mmbando
Mradi wa VSOMO ni sehemu ya mpango wa Airtel Fursa wenye lengo la kuwawezesha vijana pamoja na kutimiza kauli mbiu ya  “Airtel the smartphone network” kwa kujipatia elimu ya ufundi stadi toka VETA kwa smartphone zao” alisisitiza Mmbando
Airtel kwa kushirikiana na VETA nchini ilizindua mfumo wa masomo ya ufundi stadi kwa njia ya mtandao VSOMO Julai 2016.
Hadi sasa mfumo huu umetambulishwa  katika mikoa ya Dar es salaam, Mbeya, Arusha, Morogoro na Mwanza .

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO