Agosti 26 yaani juzi juzi hivi wapenzi wa sinema za kutisha zinazosisimua akili na kuuma meno wameshuhudia kazi nyingine ya Fede Alvares inayotisha kama jehenamu katika akili za watu, sinema inayokwenda kwa jina la Don’t Breath.
Fede Alvarez ambaye miaka michache iliyopita alitengeneza upya sinema iliyotisha akili ya Evil Dead, kuja kwake na sinema hii kunaonesha ni kwa namna gani anafanikiw akucheza na hofu za wanadamu.
Kartika simulizi hili la kutisha la Don’t Breathe binti mdogo (Jane Levy, ambaye pia aliigiza katika sinema ya Alvarez ya Evil Dead)  anakubaliana na shauri la mpenzi wake na rafiki yake la kumaliza tatizo lao la fedha kwa kufanya ujambazi katika nyumba ya mtu mmoja asiyeona.
Lakini  wao bila kujua wakawa wameingia katika balaa kubwa kwani mzee huyo badala ya kuwafukuza watoke katika eneo lake anaamua kuwaua  na katika hilo dahh, kama hujaenda haja ndogo unaweza kujisaidia ukiangalia picha hii inavyokuchukua katika hofu kubwa kama sio kuu ya roho na maisha yako.
Ukiangalia trela unaona jinsi  mtengenezaji wa filamu hii anavyokufanya uamini kwamba ni wewe unapambana na madhila yale ambayo yanakufanya ukose raha tangu unaingia mpaka unatoka.
Ni kweli kabisa marafiki watatu (Dylan Minnette, Jane Levy na Daniel Zovatto)  juhudi zao za kutaka kunukisha kwa fedha za wizi zinagonga ukuta mpaka wanataka ardhi iwameze jinsi wanavyohangaika katika kujaribu kuokoa maisha yao.
Sehemu  njema kabis aimechezwa na huyu mzee kipofu, nafasi iliyochezwa na Stephen Lang,ukimuona  unadhani kweli ni mtu ambaye ni m pole na asiyeona kumbe ana siri kubwa anaificha na ndipo unapojua kumbe kurukaruka kwa maharage ndio kuiva kwake.
Mtu mmoja akizungumzia sinema hii alisema kwamba ni moja ya masimulizi yenye kuleta msisimko mkubwa katika akili na mwili kiasi cha kutetemeka ingawa imefanyw ana watu wale wale wanaojua.

y Drebe73 akiandika katika uhakiki wake alisema kwamba sinema imetengenezwa vizuri, simulizi ni nzuri na pia walioigiza wamefanya vyema hasa katika maeneo ambayo yamedhamiria kuingiz ahofu katika akili ya mtazamaji .

Anasema ni vigumu sana kuelezea vyema simulizi hili jinsi lilivyokuwa safi na lenye uhakika na kwamba alikuwa anatetemeka wakati akiangalia sinema hiyo.

Anasema moyo hupiga kwa nguvu ukitazama sinema hiyo na kusema kwamba ilimeletea alama isiyosahaulika katika akili yake na kwamba hakika jina la sinema limeshabihi sana mambo yaliyomo ndani hata wewe unayetazama unabana pumzi kwa hofu.

Anasema kwamba sinematografia iliyofanyika katika sinema hii ni bomba na uigizaji ulikuw atimamu sana na ni sinema ya kuiona.

Darekta Fede Alvares ambaye filamu yake ya  2013 ya Evil Dead, ilikuwa na mafanikio makubwa amefanya kinyume na madarekta wengi ambao hutafuta picha yenye malipo makubwa zaidi, lakini yeye ametengeneza sinema yenye bajeti ndogo lakini inayokoza kama titi la mama.
Darekta huyu mwenye asili ya  Uruguaya  anawatwaa Stephen Lang ( aliyekuwa katika Avatar ) na  Jane Levy (Evil Dead, TV's Suburgatory) kufanya  Don’t Breathe inayochanganya wapenzi wa sinema za kutisha.
Sinema hii ambayo ilioneshwa mara ya kwanza (primia) katika tamasha la SXSW mapema mwaka huu imeingia katika majumba ya sinema Agosti 26 na kumuonesha  Alvares kwamba anayamudu majambo haya ya kutisha watu.
Mwenyewe anasema kwamba mafanikio yake yanatokana na nia yake ya kila siku kutoingia katika filamu za bajeti kubwa.Anasema yeye  anaamini kwamba ni vyema kuwa na stori inayosimulika na watu wanaojua kuwasilisha simulizi hilo kuliko fikira za Hollywood za kutengeneza picha zenye gharama kubwa baada ya kuona ya kwanza imefanya vyema. Anasema baada ya Evil Dead walimtaka atengeneze sinema ya bajeti kubwa akagoma.
Alvarez anasema maamuzi yake yalitokana na kufahamu kwamba kukimbilia vitu vikubwa kunaweza kuleta athari kwako hasa katika kuwezesha  mazingira yanayoweza kukufanya kutoa kitu bora nah ii ndio ilimfanya kukaa kimya na kuja na sinem a hii nyingine baada ya muda mrefu sinema ambayo ni bajeti ndogo.
Alvarez anaamini kwamba sinema yake itakuwa bora kwa kuwa ina grafiki kidogo na sehemu kubwa imefanyika kiukweli na dahh kukufanya usikea vyema katika kiti chako.
Alvarez anasema kwamba wazo la kutengeneza sinema hiyo liklitokana na maongezi tu kuhusiana na wizi. Simulizi la aina hii lina mkanganyiko mwingi na wa aina tofauti ambao wananchi wanaojua wapo wezi wengi hawakamatwi hawaonwi na wanaendelea na maisha . pamoja na kuchukia wizi lakini wengi wao wanadhani kwambna wanaweza kuishi wka staili hiyo ndipo ikaja simulizi hiyo kama changamoto, na kubwa zaidi tuliamua kwamba mtu wetu awe kipofu.
Mimi naamini kwamba Alvares amefanikiwa kwa mara nyingine tena kusisimua wapenzi wa sinmema za kutisha na katika hili nampa saluti. Je una kitu unataka kujua au kusimuliwa? Niandikie katika SMS 0713176669 au msimbebeda@gmail.com

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO