WATU wanne wamekufa na wengine sita kujeruhiwa baada ya basi la  kampuni ya JM Luxury kuligonga lori lililokuwa likikata kona kuelekea kishapu.
Ajali hiyo imetokea Njiapanda ya Kolandoto.
Kaimu kamanda wa polisi mkoani Shinyanga Elias Mwita alisema ajali hiyo ya basin a lori Lori linalomilikiwa na kampuni ya Birichand aina  Tata  lenye namba  za usajili T218 ABY ilitokea saa 11 .15 alifajiri  na imesababishwa na dereva wa basi la JM Luxury ililokuwa likielekea  Mwanza. Majeruhi wanne walilazwa hospitali ya Kolandoto ni  Salehe Kassimu ambaye ni dereva wa basi  (46),Mohamed   Ahamed (39) ambaye ni kondakta na Valencia Magingi (34) abiria  na waliolazwa hospitali ya  mkoa ni Joseph Mkunda (58) na Salome Paulo  na mmoja hajatambulika.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO