MGOMO wa magari ya kusafirisha abiria maarufu kama daladala uliodumu
takribani saa saba umesababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi wa Mji
wa Dodoma hali iliyowalazimu baadhi ya watu kutembea kwa miguu huku
wengine wakipanda pikipiki na bajaji. safari fupi ilifanywa kwa shilingi kati ya elfu moja na mbili
Daladala zilisusia kutoa huduma  ya kusafirisha abiria leo asubuhi kwa madai
ya kuchoka kunyanyaswa na Askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoani
hapa.
Hali hiyo ilisababisha Mkuu wa wilaya ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na  usalama ya Wilaya   Mjini, Christina Mndeme kuitisha
kikao cha haraka na madereva, pamoja na  Jeshi la Polisi  kikosi cha
usalama barabarani  ili kuweza kupata  mwafaka.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti  kwenye mkutano huo baadhi ya
madereva na wamiliki wa daladala walidai kuwa sababu kuu ni kutozwa
faini nyingi zisizo na maelezo na kudhalilishwa.
Akijibu tuhuma hizo Mkuu wa Kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa
Dodoma Marison Mwakyoma alisema hakuna sheria inayomruhusu  Askari
kumnyanyasa Dereva ila kinachotakiwa kufanyika ni kuelezwa kosa alilofanya kabla ya kutozwa adhabu.
Mwakyoma alisema kuwa wamekuwa wakiwakamata madereva hao  kutokana na
kuvunja sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamojana na kujaza
abiria na kuwasimamisha ,uchakavu wa magari na kutokuwa na leseni
inayowaruhusu kuendesha magari ya abiria.
Akizungumzia vituo vya kupakia na kushusha abiria aliomba kufuatana na
Uongozi wa Wenye daladala na Madereva ili kuangalia na kuainisha vituo
vinavyotakiwa ili kuweza kutoa maagizo kwa Askari wake wasiwakamate
wanaposimama maeneo hayo.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Christina Mndeme aliwaagiza Uongozi wa
manispaa ya Dodoma kuweka vibao kwenye vituo vitakavyoaanishwa
kushusha na kuapakia abiria.
Mndeme aliwaomba madereva hao kuwasiliana na uongozi wa Serikali
wanapokuwa na malalamiko yoyete ili kuondoa usumbufu kwa Wananchi
wanaopata huduma ya usafiri huo.
Kwa upande wake,Ofisa wa Usimamizi wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu
(Sumatra) Henry Simba alisema kwa upande wao hawako tayari kuwavumilia
madereva wanaovunja sheria ya kupakia abiria kuzidi idadi inayotakiwa
.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO