MUIGIZAJI wa filamu za aksheni  ambaye pia ni projuza na dairekta Jackie Chan anatarajiw akupewa tuzo ya Oscar ya heshima kutokana na mafanikio yake makubwa katika tasnia ya filamu. 

Taasisi inayotoa tuzo hizo ya Academy of Motion Picture Arts and Sciences pia imesema itampa tuzo ya heshima ya Oscar kwa Mhariri wa sinema wa Muingereza Anne V Coates, darekta anayesaka waigizaji Lynn Stalmaster  na mtengeneza dokumentari Frederick Wiseman.

Rais wa taasisi hiyo Cheryl Boone Isaacs amesema kwamba wanaopewa tunzo hizo wanastahili kupewa kutokana na jinsi walivyo mahiri katika kazi zao.
Watu hao watapewa tunzo hizo Novemba 12 mwaka huu .
Chan, 62, ambaye ameshiriki kama muigizaji katika lukuki za sinema za mapigano akiwa katika ardhi ya taifa lake mjini Hong Kong ikiwamo Police Story, Armour of God  na mwendelezo wake, alipata mafanikio makubwa kimataifa wakati alipotoka na Rumble in the Bronx, filamu za kikaragosi ya Kung Fu Panda na mtiririko wa sinema za Rush Hour.
Pia mkali huyu wa sinema za Kung Fu  ambaye hucheza maeneo ya maigizo yenye hatari yeye mwenyewe, amekuwa akiandika filamu kuongoza (darekta) , kuzalisha (projuza) na kufanya koregrafia kwa sinema nyingi ambazo zimezalishwa naye.
Kwa mujibu wa taasisi ya Academy, mkali huyo amekuwa kwa miongo minne akiburudisha wapenzi wake katika hali bora kabisa.
Baada ya kutolewa kwa taarifa hiyo Chan alitoa shukurani kwa familia yake, mashabiki na watoa tunzo.
Aliandika katika ukurasa wake kwamba anawashukuru watu wa Academy kwa kumpatia Oscar angali kijana , huku kijana akiiwekea mabao.
Alisema anajisikia kuheshimika sana kuwa Mchina wa kwanza katika historia kupewa tunzo ya Oscar.
Aidha alisema kwamba kutengeneza filamu za mapigano si rahisi na mara nyingi wanaumia na kusema tuzo hiyo atawapa pia timu yake ya uigizaji maeneo ya hatari ya JC Stunt.
Alisema pamoja na kupewa tunzo hiyo atapigania kupata nyingine.
Naye Anne V Coates aliyezaliwa Reigate , Surrey  mwaka  1925,amekuwa katika masuala ya filamu kwa miaka 60 kama mhariri wa filamu na kupata tunzo ya Oscar kutokana na kazi yake ya mwaka 1962 ya Lawrence of Arabia.
Sasa akiwa na miaka 90, amefanyakazi na Fifty Shades of Grey, filamu yenye mafanikio makubwa ya iliyotokana na kitabu cha EL James  kilichouzwa sana.
Naye Lynn Stalmaster akiwa amezaliwa Omaha, Nebraska mwaka 1927, ametia mkono wake katika kutafuta waigizaji katika sinema zaidi ya 200 ikiwamo The Graduate and Deliverance.
Wakati huo huo Frederick Wiseman, ambaye anaaminika kufanya sinema akila mwaka toka mwaka 1967  ikiwamo ya saa tatu ya mwaka 2014 ya National Gallery  huko London.
Imeelezwa kuwa tunzo hizo zinafikishwa kwao kutokana na wao kuwa watu wa aina yake waliowezesha mafanikio makubwa katika tasnia ya sinema kutokana na vipaji vyao na matumizi ya akili zao kwa kiwango cha hali ya juu.
Mwaka jana waliopata tunzo hizo za heshima ni pamoja na Spike Lee na muigizaji wa kike Gena Rowlands

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO