Angelina Jolie (41)amefikisha shauri la kutaka talaka kutoka kwa mume wake Brad pitt (52).
Imeelezwa kuwa kuachana kwao kunatokana na tofauti namna ya kulea watoto wao.
Kwa mujibu wa TMZ talaka hiyo inatokana na Jolie kusikitishwa sana na namna ambavyo pitt anaendesha ulezi katika familia hiyo.
Picha yao ya mwisho kutengeneza pamoja ni ile ya By the Sea mwaka jana na ilikuwa inazungumzia mvurugiko katika ndoa
Ndoa yao ilifanyika Agosti 2014 , miaka kumi baada ya kuanzisha kwa mahusiano yao wakati wakicheza sinema ya Mr. and Mrs. Smith ambapo Pitt alikuwa bado yuko katika ndoa na Jennifer Aniston.
Wawili hao walioana kisheria mjini Califonia kabla ya ndoa yao iliyopangwa na watoto mwaka 2014 na ndipo hapo hapo Jolie alipoombea talaka akidai tofauti ambazo haziwezi kumalizwa.
 Kabla ya kuolewa na Pitt,Jolie,alishawahi kuolewa mara mbili.


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO