Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria na nahodha wake Kanu Nwankwo  amefiwa na mama yake.
Imeelezwa kuwa mchezaji huyo gwiji ambaye amestaafu kucheza mpira alifiwa mama yake, Susan Kanu Iheme, Septemba 7 mwaka huu.
Tayari washabiki katika mtandao wa Facebook  wameanza kumpa pole.
Haijajulikana bado sababu ya kifo cha mama huyo wa Kanu Nwankwo  ambaye alikuwa ameelezwa na mwanae kabla hajawa staa wa kimataifa kwamba atamfanya kuwa mmoja wa wanawake wenye furaha sana duniani kutokana na kusukuma kwake ndinga.
Kanu wakati akicheza soka alikuwa pande za ushambuliaji (fowadi)  na baadae kuwa kapteni wa timu ya taifa ya Nigeria kwa miaka 16 kuanzia 1994 hadi 2010.
Mchwezaji huyo mwenye mke ambaye wameishi pamoja kwa miaka 12 sasa wana watoto watatu.
Nwankwo Kanu, aliyezaliwa Agosti 1, 1976  huko  Owerri, Nigeria na akiwa na urefu wa mita 1.97  na kumuoa Amarachi mwaka 2004  akiwa na watoto watatu Iyang Onyekachi Kanu, Pinky Amarachi Kanu, Sean Chukwudi Kanu pia ana ndugu ndugu zake akina Christopher Kanu, Henry Nwosu, Anderson "Anders" Gabolalmo Kanu.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO