Kaimu Shehe wa Mkoa wa Dodoma,Ahmed Said akizungumza na Waandishi wa Habari(hawapo pichani)kuhusiana na siku ya Amani Duniani inayotarajiwa kufanyika Jumatano Mkoani Dodoma kushoto ni Akofu wa KKKT taasisi ya Dodoma kulia ni Stella Vuzo kutoka kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa.

MAADHIMISHO ya siku ya amani duniani yanafanyika kesho Septemba 21 Mkoani Dodoma ambapo mada mbalimbali zitajadiliwa huku kauli mbiu ya mwaka huu ikisema tokomeza ruswa, dumisha amani.
Akizungumza kuhusu maadhimishi hayo,Stella Vuzo kutoka kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) cha Jijini Dar es salaam alisema kila ifikapo Septemba 21 dunia inafanya maadhimisho ya siku ya amani duniani.
Alisema siku hiyo imeandaliwa kipekee ba baraza la umoja wa mataifa kwa lengo la kuhakikisha dunia inakuwa mahali salama pa kuishi, kutokomeza umaskini, kutokomeza vitendo vyote vya vya uvunjifu wa haki za binadamu na kukuza mahusiano yanayoleta na kujenga amani.
 
Ofisa Habari kutoka Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa,Stella Vuzo akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na siku ya amani Duniani inayotarajiwa kufanyika Mkoani Dodoma kulia ni Afisa Mawasiliano kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Jeremia Mwakyoma.
 Alisema  kwa Tanzania maadhimisho hayo yatafanyika mkoani Dodoma na waandaaji wa siku hiyo ni umoja wa mataifa kupitia kituo chake cha habari kwa kushirikiana na asasi nyingine zisizo za kiserikali.
Alisema lengo la kuandaa kauli mbiu ya kitaifa ni kutokana na haja ya kuelezea kiini cha migogoro mbalimbali na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini yanayotokana na  na uwepo wa rushwa iliyokithiri ambapo huchangia katika kukosa huduma sawa, migogoro ya kisiasa na demokrasia, migogoro ya wakulima na wafugaji hata mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
“Kama taifa tukiweza kuitokomeza rushwa katika jamii zetu maendeleo na ustawi wan chi utakaopelekea kuwepo kwa amani ya kudumu utakuwepo” alisema

Waandishi wa Habari wakimsikiliza Ofisa Habari kutoka Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa,Stella Vuzo(hayupo pichani) kuhusiana na siku ya Amani duniani ambayo itafanyika Jumatano Mkoani Dodoma

Ofisa Habari kutoka Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa,Stella Vuzo akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na siku ya amani Duniani inayotarajiwa kufanyika Mkoani Dodoma kulia ni Afisa Mawasiliano kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Jeremia Mwakyoma.

Alisema UN ilianzishwa ili kufanya dunia iendelee kuwa na amani  kwani bila amani maendeleo hayawezi kupatikana.
Alisema katika maadhimisho hayo kutakuwa na watoa mada ambapo wabunge mbalimbali watashiriki katika hilo pia viongozi wa dini na Jaji Sophia Wambura atatoa mada kuhusu rushwa ya ngono na jinsi jamii inavyoweza kujikinga.
Kwa upande wake kaimu Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Ahmed Saidi alisema amani ni tunu inayopatikana kutoka kwa mwenyezi Mungu.
Pia alitaka watanzania wasiweke udini na ukabila kwani kwa kufanya hivyo kutasababisha amani iliyopo kupotea”hakuna kitu kikubwa na kilicho bora kama amani tupo hapa kwa vile kuna amani tunaabudu kwa ajili ya amani kuna watu wanakuwa wakimbizi ndani ya nchi yao kutokana na kukosa amani” alisema

Source:Sifa Lubasi

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO