KIJANA mmoja wa miaka 24 ameghadhabika na kumuua mpenzi wake baada ya kufanya mapenzi.

Imeelezwa kuwa sababu ya kufanya mauaji hayo hayo ni hasira ya kuona mpenzi wake wakati wa kufanya mapenzi kuita jina la mume wake wa zamani.

Kijana huyo Fidel Lopez baada ya kufanya kitendo hicho cha mauaji aliwaita watu wa huduma ya kwanza na pia polisi kwamba mpenzi wake Maria Nemeth (31) ana hali mbaya.

Hata hivyo katika mahojiano kutokana na mazingira aliyokutwa nayo mdada huyo alikiri kumuua baada ya mwanamke huyo kuita jina la mume wake wa zamani mara mbili wakati wakifanya mapenzi.

Fidel Lopez  katika simu alisema: “Hurry up, my girlfriend is in the bathroom! Like, I don’t know man, she’s not breathing! She’s gonna die, man! Come on, someone help her!” .

Taarifa zinasema kwamba tukio hilo la kusikitisha katika makazi ya jamaa hao  maeneo ya Sunrise  jimbo la Florida nchini Marekani ni za kikatili kutokana na jinsi, mwanaume huyo alivyomtendea mpenzi wake kabla ya kumtoa utumbo.

Polisi  wamesema  kwamba walipofika walimkuta Maria akiwa mtupu katika dimbwi la damu huku Fidel akilia. .

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO