KAMPUNI ya TBL Group imezidi kung’ara kimataifa kutokana na na viwanda vyake vya bia nchini kushinda tuzo za juu za kimataifa za SABMiller Afrika kwa uzalishaji bora, huku bia ya Safari Lager ikitangazwa bia bora barani Afrika.

SABMiller imekuwa na utamaduni wa kushindanisha viwanda vyake vilivyopo katika nchi mbalimbali lengo likiwa kuona ubora wa bidhaa zake.

Hafla ya kutangaza viwanda vilivyoshinda na kupatiwa tuzo ilofanyika juzi Afrika Kusini na kuhudhuriwa na maofisa waandamizi wa kampuni hiyo wa viwanda vya bia kutoka kampuni zake tanzu za sehemu mbalimbali duniani.

Katika hafla hiyo, bia ya Safari inayozalishwa na viwanda vya TBL vya Dar es Salaam na Arusha ilitangazwa bia bora barani Afrika na kutunukiwa huko, hukuhuku kiwanda cha Dar es Salaam kikishika nafasi ya kwanza na kile cha Arusha kikishika nafasi ya pili.

Tuzo nyingine ambazo viwanda vya TBL vimeshinda ni za uzalishaji wa bia bora ya Castle Lager ambayo imeipa TBL Dar es Salaam nafasi ya kwanza, huku TBL Mbeya ikishinda nafasi ya pili na TBL Arusha nafasi ya tatu.

Aidha, TBL Mbeya imeibuka mshindi wa upishi bora wa bia ya mwaka huku nafasi ya pili ikishikwa na TBL Mwanza ambayo pia imeshinda tuzo ya kufuata kanuni bora ununuzi na ugavi.

Akizungumzia tuzo hizo, Mkurugenzi wa Ufundi wa TBL, Gavin van Wijk amevipongeza viwanda hivyo, akisema; “Ushindani ulikuwa mkubwa ukihusisha vowanda vingine kutoka nchi mbalimbali barani Afrika.

Inafurahisha kuona viwanda vya Tanzania vinachomoza na kushinda tuzo kama hizo, hii inadhihirisha kuwa TBL imejipanga kwenda sambamba na mkakati wa Serikali wa kuifanya nchi kuwa ya viwanda.

Pia amewashukuru Watanzania kwa kuiunga mkono TBL na bidhaa zake, huku akiahidi kampuni hiyo itaendelea kuzalisha bidhaa bora na kwamba itaendelea kujikita katika kusaidia miradi mbalimbali ya kijamii ili kuboresha Watanzania kupitia sekta za kilimo, elimu, mazingira na afya.

Alisisitiza kuwa, pamoja na kusaidia katika sekta hizo, itaendelea kuwa mlipa kodi mwaminifu kwa serikaloi ili kusaidia kuinua uchumi wa nchi kama inavyosisitizwa na Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli.

Naye Meneja wa TBL Dar es Salaam, Calvin Martin, kwa niaba ya mameneja wa viwanda vya TBL nchini, ameelezea kufurahishwa kwake na mafanikio ya viwanda vya TBL katika anga za kimataifa.

Wakati huohuo, Mhandisi raia wa Tanzania, Richmond Raymond ambaye ni Meneja wa TBL kiwanda cha Mwanza, amehamishiwa Afrika Kusini kukiongoza kiwanda cha bia cha Polokwane, huku akituzwa tuzo ya heshima ya kampuni mama ya SABMiller.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO