JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI

TAARIFA KWA UMMA

Tarehe 20 Julai, 2016, Wizara ya Nishati na Madini ilitoa Tangazo kwa Umma kuhusu Kukaribisha Maombi ya Ruzuku Awamu ya Tatu kwa Wachimbaji Wadogo wa Madini nchini.
Fomu za maombi ya ruzuku hiyo zilitolewa katika Ofisi za Madini za Kanda (ZMO) na Mikoa (RMO) zikiambatana na vipeperushi maalum vinavyoeleza mambo yote yanayohusu ruzuku. Fomu hizo zilianza kutolewa tarehe 20 Julai, 2016 na ukomo wake ulikuwa tarehe 9 Agosti, 2016, saa 9:30 Alasiri. 
Wizara inatoa taarifa kuwa, imesitisha kwa muda utoaji wa Ruzuku Awamu ya Tatu ambao ulikuwa umepangwa kufanyika tarehe 19 Septemba, 2016, hadi pale Tathmini ya fedha ya Ruzuku Awamu ya Kwanza na ya Pili itakapofanyika.
Aidha, tathmini hiyo itafanyika sambamba na uhakiki wa shughuli za Wachimbaji Wadogo walioomba Ruzuku ya Awamu ya Tatu, lengo likiwa ni kujiridhisha kama Ruzuku hizo zimetumiwa na walengwa kwa malengo yaliyokusudiwa.
Imetolewa na;
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
Tarehe 16 Septemba, 2016

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO