IDARA ya Afya ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma imeifungia zahanati moja binafsi kwa kutoa huduma chini ya viwango.

Afisa Habari wa Manispaa ya Songea Albano Midelo ameiitaja zahanati hiyo kuwa ni Songea Private Dispensary.
Midelo amesema Idara ya Afya ya Manispaa hiyo ilifanya ukaguzi katika zahanati za Manispaa hiyo na kubaini dosari katika zahanati hali iliysababisha kuzifungia.

Sababu nyingine ambazo zimesababisha kufungwa kwa zahanati hizo ni kufanya shughuli ambazo haziendani na Miongozo ya Wizara ya Afya,Ustawi wa Jamii, Wanawake, Jinsia,Wazee na Watoto,kutokuwa na ikama ya watumishi ya kutosha na kukosa watumishi wenye sifa.

“Zahanati hizo zimefungiwa kutoa huduma katika Manispaa ya Songea hadi hapo zitakapokidhi vigezo vya kuendesha huduma ya afya kulingana na miongozo ya Wizara husika’’,alisisitiza Afisa Habari huyo.

Naye Mganga Mkuu wa Manispaa ya Songea Dk.Simon Chacha amesema mashine za kuzibia meno katika kituo cha afya Mjimwema hazifanyi kazi hali inayoathiri utoaji wa huduma kwa wagonjwa wa meno.

Amesema mawasiliano yamefanyika kati ya Mratibu wa Huduma za Meno na kitengo cha MOI ili kuweza kutoa fedha  za  matengenezo ya vifaa vya kituo hicho.

Hata hivyo amesema huduma za meno zimeendelea kutolewa katika vituo vingine vya kutolea huduma za afya vya serikali na baadhi ya vituo binafsi.

Dk.Chacha amesema Idara ya Afya ya Manispaa hiyo pia imekagua maduka 18 ya vyakula ambapo dosari ya kutokamilika kwa matengenezo imeonekana katika duka moja la vipodozi na bekari moja na kwamba wamiliki wamepewa ilani ya kukamilisha matengenezo ya maduka yao kabla ya kupewa kibali.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO