Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akitoa ufafanuzi  kuhusu  shughuli zinazofanywa na  kampuni  za utafiti na uchimbaji wa gesi na mafuta nchini
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa kampuni za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi nchini zinatarajia kuanza ujenzi wa mtambo wa kusindika  gesi kimiminika (Liquefied Natula  Gas; LNG) mara baada ya kukamilika kwa  taratibu za kisheria.
Profesa Muhongo aliyasema hayo jijini  Dar es Salaam kwenye majumuisho ya kikao cha siku mbili kilichokutanisha kampuni zinazojihusisha na shughuli za utafiti na  uchimbaji wa mafuta na gesi  nchini pamoja na wataalam wa Wizara ya Nishati na Madini. 
Alitaja kampuni zizakazojihusisha na ujenzi wa mtambo huo kuwa ni pamoja na Satoil ya  Norway,  Exxmobil ya Marekani,  Shell ya  Uholanzi, BG na   Ophir za  Uingereza na  Pavillion ya  Singapore.
Alisema kuwa  Wizara imeweka utaratibu wa kampuni zinazojihusisha  na utafiti na uchimbaji wa gesi na mafuta nchini kukutana kila baada ya miezi mitatu kwa ajili ya kujadili maendeleo na changamoto za shughuli zake.
Aliongeza kuwa Serikali ipo tayari  hushirikiana na  kampuni zote kupitia kubadilishana uzoefu kupitia wataalam wake lengo likiwa ni kuongeza kasi ya utafiti  na uchimbaji wa gesi na mafuta nchini pamoja na ujenzi wa mtambo wa kusindika gesi kimiminika.


Source: Greyson Mwase

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO