KATIKA kuhakikisha kuwa watanzania wanakuwa na simu zenye uwezo mkubwa ili kutanua shughuli zao za kujitafutia kipato kwa njia ya mawasiliano kampuni ya simu ya Airtel imetangaza kuendesha gulio kubwa la simu za kisasa kila Jumamosi na Jumapili.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika katika kampuni hiyo , gulio hilo kubwa litakuwa linafanyika ndani ya Mlimani City.
Akizungumza kuhusu gulio hilo ambalo limebatizwa jina la Smartphone Bazaar, Ofisa Bidhaa na Masoko wa Airtel,James Kagashe, alisema pamoja na mauzo ya simu za kisasa aina ya fero 280, Magnus Z11 na Huawei Y3C pia wana simu aina ya Samsung na Techno.
“ Tunayofuraha kuwaletea sokoni wateja wetu simu za kisasa , origino na zenye gharama nafuu hadi shilingi 24,000. Tunazo simu nyingi ikiwemo simu Aina ya fero 280 inayouzwa 24,000, simu ya smartphone aina ya Magnus Z11 inayouzwa kwa shilingi 83,000 na simu ya Huawei Y3C kwa shilingi 140,000, ” alisema Kagashe.
Aliwataka wananchi wanaotaka kufaidika na elimu mbalimbali zinaoztolewa kwa njia ya simu za mkononi kwenda kununua simu hizo za kisasa.
Aidha alisema kwamba katika gulio hilo pia watakuwa na simu za kisasa za bei nafuu zaidi ili kuwawezesha wateja kujiunda na  kampeni ya Sibanduki yenye lengo la kusogeza huduma za mawasiliano ya simu karibu na wananchi.
Huduma hizo ni pamoja na kutuma na kutoa pesa bure, kujitengenezea vifurushi vya yatosha na kupata MB zaidi, SMS zaidi na intaneti zaidi,  kupata mikopo ya Timiza isiyo na dhamana, kutoa pesa benki na kuweka kwenye akaunti zao za Airtel Money wakati wowote.
Aidha wateja wapya watapata vifurushi vya dakika 60, SMS 2000 na MB 200 bure bila , vifurushi hivi vitadumu kwa muda wa siku 60.
mwisho

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO