Watoto  nane  wakiwemo wanne wa familia wamefariki dunia na mmoja kufuatia nyumba waliyokuwa wamelala kuwaka moto baada ya waazi wa  watoto hao  kutokuwepo nyumbani kufuatia kuhudhuria sherehe ya harusi nyumbani  jirani kijijini hapo. 
Kamanda wa polisi mkoa Kigoma,Ferdinand Mtui akizungumza na waandishi wa habari mjini Kigoma alisema kuwa watoto hao walikutwa na mauti nyumbani kwao kitongoji cha Tandala kijiji cha Chakulu wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma majira ya saa saba usiku wakiwa wamelala. 
Kamanda Mtui alisema kuwa chanzo cha moto huo ni moto uliokuwa umeweshwa kwenye jiko la mafiga lililomo ndani ya nyumba hiyo ambao ulipulizwa na upepo hivyo kushika paa la nyasi la nyumba hizo na kufanya nyumba nzima kuungua. 
Aliwataja waliofariki kuwa ni Masanja Samike (8) mtoto wa mke mkubwa, Majaliwa Samike(2) mtoto wa mke mdogo, na watoto wawili wa dada yake na mwenye nyumba ambao ni Leonald Luhende (8), Raphael Luhende. 
Aidha kwenye tukio hilo wapo watoto watatu wa jirani zake Samike John ambao walikuja kuwahifadhi watoto hao nyumbani hapo waweze kuhudhuria sherehe zilizokuwa zikiendelea kijijini na Kamanda Mtui amewataja watoto hao kuwa  Hamisi Bala,Jali Magere na Hamisi Bara. 
Kamanda huyo wa polisi mkoa Kigoma amesema kuwa wakati ajali ya moto inatokea mwenye nyumba Samike John hakuwepo nyumba kwa takribani siku mbili akiwa ameenda kufanya kazi za vibarua na kuwaacha wake zake kutunza familia.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO