Mkuu wa wilaya ya Ilemela Dkt. Leonard Masale (kulia) akipokea mbegu ya SEED.CO  mara baada ya kuzindua rasmi huduma ya bima ya kilimo ya Airtel Money Linda Mbegu .Wa kwanza toka kushoto ni mkurugenzi wa ACRE Rahab Kariuki, akifuatiwa na Meneja Mauzo wa Airtel kanda ya ziwa Emmanuel Raphael, Mkurugenzi wa kampuni ya Bima ya UAP, Raymond Kamonga, Mkurugenzi wa kampuni ya uuzaji wa Mbegu ya SeedCo Clive Mughadza na mwakilishi wa mamlaka ya Bima, Elia kijiba.
Airtel Tanzania kwa kushirikiana na ACRE Africa, SeedCo na Kampuni ya bima ya UAP Tanzania Ltd imezindua huduma ya kwanza na aina yake ya bima ya kilimo ijulikanayo kama “Airtel Money Linda Mbegu”   itakayowawezesha wakulima Tanzania kukatia bima mbegu zao za mahindi kupitia mtandao wa simu nchini.

Tanzania inategemea sana kilimo katika uchumi na chakula kwa watu wake. Sekta ya Kilimo ndio inayoajiri zaidi Tanzania, takribani 80% ya watanzania wanajishugulisha na shughuli za kilimo. Pamoja na hivyo, wakulima wachache sana wanatumia mbegu bora kwa sababu hawana uhakika na uzalishaji wa mazao yao .  kutokana  takwimu za hivi karibuni kwenye repoti ya National Bureau statistic (NBS) zinaonyesha kwa kipindi cha tangu (januari hadi Juni 2016) shughuli za Agro agricultural ambazo zinausisha kilimo, ufugaji , uvuvi na misitu zinachangia trillion 11.7 za pato la taifa ambapo asilimia 3.4 inatoka kwenye kilimo.

Akiongea  wakati wa uzinduzi wa huduma ya Linda Mbegu, Mkurugenzi wa Seed Co bw Clive Mughadza  alisema ”Kwa wakulima wadogo Tanzania, msimu mmoja mbaya wa kilimo unapelekea hasara kubwa hivyo Huduma ya Linda Mbegu inahakikisha iwapo kutatokea tukio la mvua kuwa kidogo, na mbegu kushindwa kuota,  mkulima atafidiwa mifuko mipya ya mbegu toka kwa muuzaji wa pembejeo aliyekaribu nae ili kuweza kupanda tena katika msimu ujao wa kilimo”.

Aliongeza kwa kusema” Linda Mbegu kwa sasa itawafaidisha wakulima wa Kagera, Shinyanga, Mara na Mwanza ambapo mteja atakaponunua mfuko wa mbegu atapata fursa ya kujiandikisha kwa kupiga *150*60# kisha kuingiza namba maalumu akakayoipata kwenye kikadi kilichoko ndani ya mfuko wa mbegu bila kulipia gaharama yoyote. Huduma hii itadumu ndani kwa siku 21 tu toka mkulima asajiri kadi yake”

Akiongezea, mkurugenzi wa ACRE Africa, Rahab Kariuki alisema “tunafuraha sana kuona wakulima Tanzania wakipata bima, ambayo ni yakwanza ya aina yake hapa nchini Tunamatumaini kwamba wakulima watatumia nafasi hii kulinda uwekezaji wao kwenye kilimo. Dhamira na jukumu letu la msingi sisi kama ACRE Africa ni kuwalinda wakulima dhidi ya majanga ya hali ya hewa na tunatarajia kutoa ufumbuzi zaidi wa namna ya  kukabiliana na hatari zinazowakabili wakulima katika kilimo”

Kwa upande wake, Meneja wa Biashara wa Airtel kanda ya Ziwa, Ezekieli Nungwi alisema “Airtel Tunayo dhamira ya  kuwawezesha na kuwasaidia wakulima Tanzania kwa kupitia huduma na bidhaa yenye ubunifu mkubwa kupitia huduma yetu ya Airtel money.  tunashuhudia nguvu ya technologia na jinsi huduma za simu za mkononi zinavyoweza kuchangia katika kuinua kilimo.  Wakulima sasa wanaweza kuweka bima ya mazao yao na pia kulipwa fidia zao kupitia huduma ya Airtel Money.. Tunauhakika kwamba ushirikiano huu leo utaleta hamasa katika shuguli za kilimo na kuinua vipato na uchumi wa jamii na nchi kwa ujumla"

Kwa upande wake  Mkuu wa Mkoa John Mongella alisema, ‘Wote ni mashahidi namna gani sekta ya kilimo inavyochangia katika uchumi na ukuaji wa taifa letu; Wakulima wanamchango mkubwa sana katika jamii yetu. Hata hivyo kilimo kinachangamoto nyingi, mkulima anaweza kufanya kila kitu sawa lakini majanga ya asili yakamwangusha. Tukiwa tunatambulisha bima ya kilimo leo kupitia ushirikiano kati ya  Airtel, ACRE Africa, SeedCo na Kampuni ya bima ya UAP Tanzania Ltd tunarejesha matumaini kwa wakulima wadogo,  tuhakikisha usalama na uhakika wa mitaji yao

“Nawashukuru wadau wote kwa kuanzisha Bima ya kilimo, nawaomba wakulima wa shinyanga, Mara,Mwanza na kagera kutumia fulsa hii ya kipekee kwa kujisajiri kwa wingi bila gharama yeyote ili kunufaika na mpango huu wa kipekee  “aliongeza Bwa. Mongella.

Uhusiano kati ya Airtel na SeedCo umewezeshwa na Kampuni ya bima ya UAP Tanzania Ltd  na Acre Africa ambao ni wataalam wa kutengeneza na kusimamia bima za kilimo Africa na ndio wasimamizi  wa huduma ya Linda Mbegu.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO