Mbunge wa jimbo la Nzega Mjini Mhe, Hussein Bashe (kushoto) akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso (kulia)  wakati alipotembelea ofisi za Airtel juu ya program ya WanaNzengo Airtel FURSA inayowawezesha vijana wajasiriamali waishio katika kata 10 zilizoko ndani ya Jimbo la Nzega Mjini mkoani Tabora kupata mikopo yenye riba nafuu. 

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mfuko wake maalumu wa kusaidia jamii wa Airtel FURSA Tunakuwezesha jana imekabidhi hundi ya shilingi milioni 20 kwa Mbunge wa Nzega .

Akikabidhi hundi hiyo Mkurugenzi mkuu wa Airtel , Sunil Colasa alisema “Airtel imejipanga kwa kuhakikisha vijana wanaendelea kunufaika na mradi wa Airtel FURSA kwa kuwapatia misaada ya kukamilisha mipango yao waliyoipanga kwa kupunguza changamoto walizonazo ikiwemo ya ukosefu wa ajira na  mtaji ili watimize malengo yao katika biashara”

“Tunaamini kupitia ushirika wetu na Mbunge wa Nzega, Hussen Bashe mfuko wa  Nzega Trust Fund utasaidia wananchi ndani ya vijiji 21 katika jimbo hilo ambapo malengo yetu ni kufanya mradi huu kuwa endelevu hata kwa majimbo mengine nchini” alisema Colasa

Kwa upande wake Mbunge wa Nzega Mjini, Hussen Bashe aliishukuru Airtel nakuahidi kusimamia mradi huo wa ukopeshaji kwa ajili ya kuweza kuinua vipato vya wananchi wa Nzega kama ilivyokusudiwa.

“Nitoa wito kwa wananchi wote wenye malengo ya kujiendeleza kujitoza na kujisajili katia Mfuko wetu wa Nzega Trust Fund niliouanzisha kwa ajili ya kuhakikisha tunaungana na wadau wenye nia ya kusaidia jamii kama Airtel FURSA ili kupunguza changamoto za maendeleo kwa wananchni hasa kwa  wanaokosa mitaji ya kuendesha Miradi yao mbalimbali” alisema.

“Airtel tayari wamezikabidhi pesa hizi kwangu ambazo tutazikopesha kwenu kwa Riba ya 1.5% pale unaporejesha na faida inayopatikana bado itaendelea kuwasaidia vijana wengine watakaotaka kukopa” Alieleza Bashe.

Mradi wa Airtel Fursa umeanzishwa Mei mwaka uliopita na tayari umewafikia vijana zaidi ya Elfu tano kutoka katika mikoa kumi nchini ikiwa ni pamoja na vijana zaidi ya 100 waliowezeshwa kwa kupewa mitaji na vitendea kazi  mbalimbali

Programu hii kati ya Airtel na Nzega Trust Fund chini ya Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Hussein Bashe, itawawezesha  zaidi ya  wajasiriamali 350 kunufaika na mikopo kupitia huduma ya Airtel Money. 

Mikopo hii itatolewa kwa kikundi kilichoundwa na vijana watano ambao watapewa  mtaji kati ya shilingi  Sh 100,000 hadi 1,000,000  kulingana na mahitaji yao.

Sambamba na mikopo ya  WanaNzengo Airtel FURSA vikundi vya wajasiriamali  vitaendelea kupewa mafunzo ya ujasiriamali ikiwa ni pamoja na  namna ya kuendesha vikundi pamoja na jinsi ya kutafuta soko.
Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO