Basi la  Superfeo linalofanya safari toka Mbeya kwenda Mbinga limepata ajali katika kijiji cha Gumbiro wilaya  ya Songea majira ya saa nane mchana.
Mtu  mmoja mwanaume amekufa katika ajali hii na majeruhi 12 wamekimbizwa hospitali  ya Rufaa ya Mkoa Songea.

Akizungumza katika eneo la ajali Mkuu was Mkoa wa Ruvuma  Dk Binilith Mahenge amewataka madereva na wenye mabasi kuhakikishakwamba sheria za barabarani zinazingatiwa.
Aidha alionya dhidi ya tabia ya mwendo kasi unaofanywa na madereva wa  mabasi hususan kwenye maeneo yasiyo na tochi za polisi.

Amemwagiza Kamanda was Polisi Mkoa Zuberi Mwombeji kusimamia sheria za usalama barabarani ili madereva wote  wanaofanya uzembe wachukuliwe hatua za kisheria.
Kamati ya Usalama mkoa imewapa pole majeruhi na kuwashukuru wananchi wa  Gumbiro kwa kutoa msaada wa kunusuru abiria.


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO