WATAFITI wawili na dereva wa kituo cha Utafiti cha Udongo na Maendeleo
ya Ardhi cha Selian, Arusha wameuawa na kisha miili yao kuchomwa moto
atiabaada ya kuhisiwa kuwa ni wanyonya damu ambapo Jeshi la polisi
linawashikiliwa wanakijiji 30 wa kijiji cha Iringa Mvumi kuhusiana na
tukio hilo.
Kufuatia mauaji hayo ya kinyama Mkuu wa mkoa wa Dodoma Jordan
Rugimbana ametoa amri ya kuwasimamisha kazi Ofisa Utumishi wa Wilaya
hiyo na Kaimu Mkurugenzi ili kupisha uchunguzi wa tukio hilo.
Tukio hilo lilitokea Oktoba mosi mwaka huu katika kijiji cha Iringa
Mvumi tarafa ya makang’wa wilaya ya chamwino mkoai Dodoma
Watu waliouwa walikuwa kwenye gari lenye namba za usajili STJ 9570
aina ya Toyota Hilux Double Cabin mali ya kituo cha utafiti cha Udongo
na Maendeleo ya Ardhi cha Selian, Arusha ambapo gari yao  ilichomwa
moto ambapo Kati ya watu wawili waliouwa mmoja wao ni mwanamke.
Inadaiwa marehemu walivamia na wanakijiji  wa Iringa Mvumi na
kuwakatakata kwa mapanga pamoja na silaha za jadi kisha kuwachoma moto
hadi kufa.
Inadaiwa chanzo cha tukio hilo ni mwanamke mmoja Cecilia Chimanga (34)
kupiga yowe kijijini kuwafahamisha kwamba ameona watu ambao anawahisi
ni wanyonya damu (Mumiani).
Baada ya taarifa hizo kufika kijijini ndipo mchungaji wa dhehebu la
Christian Family Church aitwaye Patric Mgonela (46) alikitangazia
kijiji kupitia kipaza sauti cha kanisani kuwa wamevamiwa na wanyonya
damu ndipo wanakijiji wakaenda kuchoma gari na kuwaua na kuwachoma
moto.
Baada ya tukio hilo msako ulifanyika kwa kujumuisha askari wa kawaida
na makachero na Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na maofisa wengine wa
polisi.
Akizungumza na gazeti hili jana Kaimu Ofisa Tarafa ya Makang’wa George
Mzuri alisema
 Watafiti hao pamoja na dereva walifika kijijini hapo kufanya shughuli
zao lakini hata hivyo hawakupitia ofisini .
“Tunasikia walifika kijijini kwa ajili ya shughuli zao lakini
hawakutoa taarifa kwenye serikali ya kijiji wakawa wanatafuta njia ya
kutokea  wakafika mahali wakakuta kinamama wanaopika chumvi kwa njia
ya asili” alisema
Alisema walimua kumuita mmoja wa wanawake hao ili waweze kumuuliza
njia  lakini mama Yule alikuwa akiogopa kwa kudhani kuwa walikuwa ni
wanyonya damu.
“Mara Yule mama akaanza kupiga kelele,karibu na hapo walipokuwa kuna
kanisa ambalo huwa linatumia kutangaza watu waelekee mbugani kuna
wanyonya damu” alisema
Alisema mara baada ya wananchi hao kufika eneo la tukio walianza
kuwashambulia watu hao na kasha kuwaua na kuwachoma moto.
 Alisema juhudi za kuwaokoa watu hao ilishindikana kutokana na wingi wa watu.
Akizungumza katika eneo la tukio Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan
Rugimbana alisema wote waliohusika na mauaji hayo watachukuliwa hatua
za kisheria.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma Lazoro mambosasa alisema mpaka sasa
watu 30 wanashikiliwa na polisi wakiwemo wanaume 21 na wanawake tisa.
source:Sifa Lubasi


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO