Brad Pitt na mtalaka wake Angelina Jolie wamefikia makubaliano ya muda ambapo watoto wao sita watakuwa chini ya himaya ya mama na baba kupewa nafasi ya kisheria kwenda kuwatembelea.
Makubaliano hayo ya wiki tatu yamewezeshwa na idara ya huduma ya jamii ya Los Angeles.
Katika makubaliano hayo, kwa mujibu wa Us Weekly Jolie, 41, atakaa na watoto hao sita: Maddox, 15, Pax, 12, Zahara, 11, Shiloh, 10, na pacha Knox na Vivienne, 8 wakati mtalaka Pitt, 52,atapatiwa haki za kuwatembelea watoto lakini katika ziara zake za kwanza ataangaliwa na therapist ambaye atakuwa na mamlaka ya kumkubalia au kumkatalia kuona watoto.
Kitu kingine wawili hao watapatiwa ushauri wa kisaikolojia binafsi na baadae kifamilia wakiwa na watoto.
Kitu kingine katika makubaliano hayo ni kwamba Pitt atakuwa bila kutajhadharishwa kufanyiwa uchunguzi wa dawa za kulevya na pombe.
Imeelezwa kuwa uchunguzi wa kwanza dhidi yake alipita kwani hakukutwa na pombe wala dawa za kulevya.
Imeelezwa kuwa Jolie amefurahishwa na mpango huo uliompa mamlaka kwa watoto na sasa anataka kuwa nayo karibu kwa manufaa ya familia.
Jolie, aliomba talaka Septemba 19 akisema kwamba  hawawezi kuendelea kuishi na mumewe kutokana na sababu zisizoweza kumalizwa.
Mshindi huyo wa tuzo za Oscar alidai talaka miaka miwili tu baada ya kufunga ndoa huku akiwa ameishi na Pitt kwa miaka 12.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO