Leonardo DiCaprio (41) kwa mara nyingine tena amedhihirisha kwamba yeye na mdenishi modo, Nina Agdal (24) ni kitu kimoja baada ya kuonwa wakibusiana katika fukwe ya malibu mwishoni mwa wiki.
Hii ni baada ya kuonwa wakitembea kwapamoja katika mitaa ya New York City Septemba 29 wakiwa na mazingira ya kutulia zaidi.

Hiyo Alhamisi ya September 29 mjini New York City walibambwa wakipata chakula cha mchana pamoja eneo la Bar Pitti kabla ya kuingia mitaani.
Tangu wakati huo kumekuwepo na maneno kwamba wawili hao wanataka kufunga ndoa ya kisiri, lakini mameneja wao wamekanusha taarifa hizo.
Leo ambaye unaweza kumuita kama msela mwandamizi katika mitaa ya Hollywood na ambaye amewapa shida sana warembo toka alipocheza filamu ya Titanic kwa sasa anaonekana kuzama katika penzi la Nina Agdal.
Nina,  anasema Leo ni boifrendi mwema kabisa akimpa kampani katika mambo yake mengi na akionesha kumjali.
Na wakiwa Malibu Leonardo DiCaprio alionwa na mapaparazi akimbusu kimahaba mdenishi wake.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO