Watoto waliofanyiwa upasuaji
MADAKTARI  bingwa Montefiore Medical Center huko Bronx, Marekani wamefanikiwa kuwatenganisha pacha waliungana vichwa kwa upande wa juu baada ya operesheni ya saa 16.5.
Mpaka tunaandika taarifa hiyo shughuli ya kukamilisha operesheni hiyo zilikuwa bado zinaendelea.
Watoto hao wawili Jadon na Anias McDonald, wenye miezi mitatu ilipofika saa kumi na mbili asubuhi shughuli ya kurekebishwa pande za juu za vichwa vyao ilikuwa ikiendelea baada ya kufanikiwa kuwatenganisha.
 
Mama akiaga watoto wake
Kazi hiyo ya kuwatenganisha ilifanywa chini ya Dk James Goodrich, ambaye anaaminikwa kuwa bingwa wa upasuaji wa fuu la kichwa, ambayo imekuwa kazi yake ya saba ya utenganishaji huku aina hiyo ya upasuaji ikiwa ni ya 59 tangu mwaka 1952.
Wazazi wa pacha hao, Nicole na Christian McDonald,walilazimika kukubali watoto wao kufanyiwa upasuaji huo ingawa walitambua kwamba ama watakufa au  ubongo kupata mushkeri.
 Goodrich aliwaambia wazazi hao majira ya saa 9 alifajiri kwamba kazi imekamilikwa na mambo yapo shwari.
 Hata hivyo wazazi hao wamesema kwamba bado hawajui kitakachoendelea kwani itapita wiki kadhaa kabla ya kupewa taarifa ya maendeleo ya watoto wao.
 Familia hiyo  ya McDonalds na hospitali ya Montefiore iliruhusu Shirika la utangazaji la Marekani (CNN) kurekodi shughuli nzima ya upasuaji ya Jadon na Anias.
 Imeelezwa kuwa wazazi hao wawili Nicole na Christian kabla ya kuelezwa kuwa watoto wao walishakuwa watu wawili tofauti, Alhamisi jana ilikuwa siku yenye mzizimo mkubwa kwa upande wa wa wazazi na wataalamu wa afya.
 Wazazi bado wanajiuliza na kitete cha nini kitatokea baada ya  watoto hao kuamka bado ni tatizo kwao.
Jumla ya operesheni 4 zimefanyika ili kuwatenganisha watoto hao ikifanyika moja baada ya nyingine na kila operesheni ilikuwa na matokeo chanya. Operesheni hii ni ya mwisho.
-Source CNN.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO